Wananchi jisajilini laini zenu za simu kwa alama ya vidole kufanya mawasiliano kuwa salama -Katibu Tawala Msaidizi - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 6 December 2019

Wananchi jisajilini laini zenu za simu kwa alama ya vidole kufanya mawasiliano kuwa salama -Katibu Tawala Msaidizi


Na Chalila Kibuda, Michuzi TV ,Lindi

Wananchi wa Mkoa wa Lindi wamejitokeza katika usajili wa laini za simu kwa alama za vidole huku Wananchi hao wakipata fursa ya kupata namba za vitambulisho kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya vya Taifa (NIDA) kwa ambao walikamilisha taratibu zote za mamlaka hiyo.

Akizungumza na Wananchi wa Mkoa wa Lindi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Katibu Tawala Msaidizi Dkt.Bora Haule amesema kuwa mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ihakikishe inaongeza nguvu ya usajili kwa muda uluobaki kwani wasipofanya hivyo Wananchi watashindwa kupata mawasiliano.

Dkt.Haule amesema usajili wa laini za simu kwa alama za vidole kufanya mawasiliano yanakuwa salama kwani huduma nyingi zinafanyika kwenye simu hivyo usalama huo ni kila mwananchi asajili laini ya simu.

Amesema kuwa Wananchi wa Mkoa wa Lindi ambao hawajafanya utaratibu wa kupinga picha mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wafanye hima kuweza kupata namba au Kitambulisho kukidhi matakwa ya usajili laini ya simu kwa alama za vidole.

Aidha amesema kuwa Kampeni ya sasa mtu haachwi nyuma katika usajili kwani usajili huo serikali imewekeza kuwa bure kuondoa changamoto ya kizingizio cha fedha kuchangia Wananchi.

Nae Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Semu Mwakyanjala amesema kuwa takwimu zinaonyesha waliosajiliwa kwa alama za vidole ni zaidi ya milioni 18 na zoezi linaendelea.

Amesema kuwa serikali imewekeza fedha kwa ajili ya Wananchi wajisajili kwa mfumo wa alama za vidole.Mwakyanjala amesema TCRA iko karibu katika kuratibu ili asiweze kuachwa nyuma mtu asisajiliwe labda itokee kwa mtu mwenyewe kuwa na matatizo mbalimbali ikiwemo ya kiafya.

Mwakyanjala amesema wanafanya Kampeni katika vyombo vya habari katika kila Mkoa ili kila mtu kuweza kupata taarifa za usajili wa alama za vidole.

Nae Mratibu wa Shughuli za Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Wales Maisha amesema wanakumbana na Wananchi kujisajili mara mbili kwa majina tofauti.

Amesema kuwa wanaongeza nguvu katika usajili ili kuhakikisha kila mtu anapata kitambulisho cha taifa kwa kufuata taratibu zilizowekwa.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Semu Mwakyanjala akizungumza na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Karibu Tawala Msaidizi Dkt.Bora Haule mara baada kufungua usajili wa laini za simu kwa alama za vidole katika uwanja Fisi Manispaa ya Lindi.

Wananchi wakiwa katika foleni ya kuhudumiwa namba za vitambulisho vya Taifa katika mfumo wa Mamlaka hiyo
KatibuTawala Msaidizi wa Mkoa wa Lindi Dkt.Bora Haule akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi wakati wa Uhamasishaji wa Usajili laini simu kwa alama za vidole uliofanyika katika uwanja wa Ofisi Manispaa ya Lindi.
Mratibu wa Shughuli za Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Mkoa wa Lindi Wales Maisha akizungumza kuhusiana namna wanavyowafikia Wananchi katika usajili huo pamoja na kukutana na changamoto Wananchi kujisajili zaidi ya mara mbili uwanja Fisi Manispaa ya Lindi.
 

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Semu Mwakyanjala akizungumza na waandishi habari kuhusiana na mamlaka hiyo ilivyojipanga katika kutoa elimu ya usajili wa laini simu kwa alama za vidole tangu walivyotangaza usajili huo 
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Semu Mwakyanjala akizungumza na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Karibu Tawala Msaidizi Dkt.Bora Haule mara baada kufungua usajili wa laini za simu kwa alama za vidole katika uwanja Fisi Manispaa ya Lindi.

Wananchi wakiwa katika foleni ya kupata namba au vitambulisho vya Taifa kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad