KOMBE LA FA; YANGA DHIDI YA IRINGA UNITED KESHO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 20 December 2019

KOMBE LA FA; YANGA DHIDI YA IRINGA UNITED KESHONa Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Kikosi cha Yanga kimeendelea na mazoezi yake ya mwisho kujiandaa na mchezo wa Shirikisho Azam Confederation Cup FA dhidi ya Iringa United hapo kesho.

Yanga itaanza safari ya kutafuta nafasi ya kushiriki mashindano ya Kimataifa msimu ujao mchezo utakaochezwa majira ya saa 10 alasiri, uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Katika mazoezi hayo Beki wa Kulia Paul Godfrey 'Boxer' amerejea kikosini baada ya muda mrefu akitoka kumuuguza majeraha ya muda mrefu.

Yanga msimu uliopita waliondolewa naLipuli kwenye hatua ya nusu fainali ya baada ya kufungwa mabao 2-0.

Kaimu kocha mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya kushuka dimbani hapo kesho na wanafahamu umuhimu wa mchezo huo na wanaiheshimu Iringa United hata kama inashiriki Daraja la Kwanza (FDL).

Mkwasa amesema, anafahamu bingwa wa mashindano haya anaiwakilisha nchi kwenye kombe la Shirikisho Barani Afrika na mnapocheza hakuna marudiano atakayeshinda anaenda hatua inayofuata, wamejipanga kuhakikisha wanapata matokeo.

Mbali na mchezo huo, Lipuli watakuwa wenyeji wakiikaribisha Dar City ya jijini TangaIringa uwanja wa Samora , Dar City inashiriki Ligi Daraja la Pili (SDL).

Kagera Sugar wao watakuwa Uwanja wwa nyumbani wa Kaitaba kuikaribisha Rufiji United inayoshiriki ligi daraja la pili ambapo kocha wa timu hiyo, Mecky Mexime amesema wanauchukulia mchezo huo kwa umuhimu mkubwa kwani lengo lao ni kusonga kushinda na mbele zaidi.Kikosi cha Yanga kikiwa mazoezi leo Katika Uwanja wa Uhuru.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad