HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, December 22, 2019

CAMEL FLOUR WATOA MSAADA KITUO CHA KULELEA WAZEE KIGAMBONI NA KITUO CHA UMRA MAGOMENI


Meneja wa Biashara na Maendeleo wa Kampuni ya Camel Flour, Tawaqal Sumba akikabidhi msaada ya mifuko ya unga wa ngano (20) kwa Msimamizi wa Kituo cha Kulelea Watoto Yatima na wanaoishi mazingira magumu cha Umra Rahma Kishimba kilichopo Magomeni Jijini Dar es Salaam.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Kituo cha Kulelea Wazee na Walemavu sambamba na Kituo cha Kulelea Watoto Yatima na wanaoishi mazingira magumu cha Umra wamepokea msaada wa mifuko ya unga wa ngano kutoka kwa Kampuni ya Camel Flour.

Kampuni hiyo, imekabidhi mifuko 20 kwa Kituo cha kulea wazee na walemavu Kigamboni na Mifuko 20 kwa Kituo cha watoto Yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Umra.

Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo, Meneja Biashara na Maendeleo kutoka Camel Flour Tawaqal Sumba amesema wanashukuru kwa mapokezi mazuri waliyoyapata kutoka katika Kituo cha Wazee na Umra na wamefurahi kuo

Tawaqal amesema, huu ni mwanzo katika kurudisha walichonacho kwa jamii na wataendelea zaidi kwani huu ni mwanzo na watarudi tena.

Kwa upande wa Msimamizi Msaidizi wa Kituo cha Kulea Wazee, Frank Munuo amesema wameshukuru sana kwa msaada huo kutoka Kampuni ya Camel Flour ambapo mifuko hiyo itawasaidia katika kuendelea kuwalea wazee hao sambamba na Walemavu.

Amesema, wamekuwa wanalea jumla ya wazee 27 hadi kufikia sasa na nyumba hizo 50 ambazo zilijengwa mwaka 1973-75 na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambapo kwa sasa wanalea wazee na walemavu
Wa Ukoma, wasiosikia, wajane, wasioona na afya ya akili 

Naye Msimamizi wa Kituo cha Umra, Rahma Kishimba amesema wana jumla ya watoto 117 wanaotoka kuishi kwenye mazingira magumu wengine wakiwa ni yatima.

Amesema, katika kituo hicho wana watoto wa kuanzia miaka 2 hadi 15, wengine wakiwa wanasoma shule za Msingi na watoto wengine 7 wanaingia kidato cha kwanza mwakani.

Rahma ameeleza kuwa, msaada huo walioupata kutoka kampuni ya Camel Flour utawasaidia sana , na amewaomba makampuni mengine kujitokeza kwa bado wanahitaji msaada wao.

Aidha, Amesema mpaka sasa katika kituo chao wana changamoto ya Bima za Afya kwa watoto pamoja na vyeti vya kuzaliwa na kuwataka wadau kujitokeza kumsaidia hilo.
Meneja wa Biashara na Maendeleo wa Kampuni ya Camel Flour, Tawaqal Sumba akikabidhi msaada ya mifuko ya unga wa ngano (20) kwa Msimamizi Msaidizi wa Kituo cha Kulea Wazee na Walemavu Kigamboni Frank Munuo kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Biashara na Maendeleo wa Kampuni ya Camel Flour Tawaqal Sumba akiwavalisha khanga wazee wanaoishi kwenye Kituo cha Kulea Wazee na Walemavu Kigamboni.Kampuni ya Camel Flour imekabidhi mifuko 20 kwa Kituo hicho.
Wazee wa Kittuo cha Kulea Wazee na Walemavu Kigamboni wakiwa wanamsikiliza Msimamizi Msaidizi wa Kituo hicho Frank Munuo baada ya kupokea msaada wa mifuko 20 ya unga wa ngano kutoka Kampuni ya Camel Flour.
Meneja wa Biashara na Maendeleo wa Kampuni ya Camel Flour Tawaqal Sumba akizungumza na wazee wanaoishi kwenye Kituo cha Kulea Wazee na Walemavu Kigamboni. Kampuni hiyo imewatembelea wazee hao na kutoa mifuko 20 ya Unga wa ngano.
Meneja wa Biashara na Maendeleo wa Kampuni ya Camel Flour Tawaqal Sumba akiwa katika picha ya pamoja na wazee wanaoishi kwenye Kituo cha Kulea Wazee na Walemavu Kigamboni. Kampuni hiyo imewatembelea wazee hao na kutoa mifuko 20 ya Unga wa ngano.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad