VITAMBULISHO VYA MAGUFULI KUWAPA MIKOPO WAJASIRIAMALI WAMACHINGA BILA DHAMANA, BENKI YA CRDB YATENGA BILIONI 10 KUPITIA MIKOPO YA “JIWEZESHE” - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 6 November 2019

VITAMBULISHO VYA MAGUFULI KUWAPA MIKOPO WAJASIRIAMALI WAMACHINGA BILA DHAMANA, BENKI YA CRDB YATENGA BILIONI 10 KUPITIA MIKOPO YA “JIWEZESHE”

Wajasiriamali wadogo maarufu kama wamachinga katika wilaya ya Kigamboni sasa kuanza kufurahia mikopo kwa ajili ya kukuza na kuboresha biashara zao kupitia uwezeshaji unatolewa na Benki ya CRDB kupitia mkopo wa ‘Jiwezeshe’.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mikopo hiyo ya ‘Jiwezeshe’, Nainu Waziri Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Japhet Kandege aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuwa Benki ya kwanza nchini kuitikia wito uliofanywa na Mheshimiwa Rais wa kuwawezesha wajasirimali wadogo maarafu kama wamachinga ambao wengi wao ni vijana.

“Ni fahari sasa kuona vitambulisho vya Magufuli, vikizidi kuleta neema kwa wajasiriamali wetu wamamchinga kupitia mikopo hii ya ‘Jiwezeshe’ kutoka Benki yetu ya CRDB. Salamu hizi mlizotuletea Benki ya CRDB tutazifikisha kwa Mheshimiwa Rais kumueleza namna ambavyo mmemuunga mkono,” alisema Naibu  Waziri Kandege.
Kwa upande wake, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Benard Kibesse aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuwa Benki ya kwanza nchini kutoa mikopo kwa wajasiliamari wadogo bila riba. “CRDB mmeomyesha njia kuwa hili linawezekana. Mwaka huu mmeanza na wajasiliamari 3,000, nawapa changamoto kuwa mwakani tukikutana kama hivi, muwe mmeshatoa mikopo kwa wajasiliamari 10,000” alisema Dkt.Kibese.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema mikopo hiyo ya ‘Jiwezeshe’ inatolewa kidijitali kupitia huduma ya SimAccount ambapo wateja wataweza kukopa kuanzia kiasi cha shilingi 10,000 hadi shilingi 500,000 kupitia simu zao za mkononi.
“Mjasiriamali anatakiwa kufungua SimAccount kwa kupiga *150*62# na kisha kujisajili kutumia kitambulisho chake cha ujasiriamli, ambapo ataweza kunufaika na mkopo binafsi wa ‘Jiwezeshe’ au kupitia kikundi,” aliongezea Nsekela.

Nsekela alisema kwa kuzingatia mazingira ya biashara za wajasiriamali wamachinga, Benki ya CRDB imeachana na mpango wa kutoza riba kwa asilimia na badala yake mteja atatozwa kiwango kidogo cha kati ya shilingi 5,00 na 2,000 tu pindi arejeshapo mkopo.

“Tumefanya hivi ili kuwapunguzia mzigo wajasiriamali hawa wadogo, ili waweze kuwekeza zaidi faidi wanayoipata kupitia mikopo hii ya ‘Jiwezeshe’,” alisema Nsekela.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sara Msafiri aliwahamasisha wajasiriamali wadogo katika wilaya hiyo kuchangamkia fursa hiyo ya mikopo ya ‘Jiwezeshe’ kwa kujiunga na huduma ya SimAccount ya Benki ya CRDB.

Kupata maelezo zaidi juu ya mikopo ya ‘Jiwezeshe’ tembelea www.crdbbank.co.tz
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati wa Uzinduzi wa Mikopo ya kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wa Kigamboni, iliyofanyila leo katika Ukumbi wa Kibada Garden, jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Naibu Waziri wa TAMISEMI ambaye pia alikuwa Mgeni Rasmi kwenye hafla hiyo, Josephat Kandege (wa pili kushoto) pamoja na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Bernard Kibese (kulia).
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa akizungumza wakati alipokuwa akiongoza katika hafla ya Uzinduzi wa Mikopo ya kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wa Kigamboni, iliyofanyila leo katika Ukumbi wa Kibada Garden, jijini Dar es salaam. 
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad