TIMU YA KILOMBERO SOKA NET ACADEMY KUCHEZA NA MPWAPWA MJI KOMBE LA ASFC JUMAMOSI HII - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 28 November 2019

TIMU YA KILOMBERO SOKA NET ACADEMY KUCHEZA NA MPWAPWA MJI KOMBE LA ASFC JUMAMOSI HII


Na Farida Saidy, Globu ya Jamii
TIMU ya Kilombero Soka Net academy ya Ifakara mkoani Morogoro imekamilisha maandalizi yake ya michuano ya Azam Federation inavyoendelea hivi Sasa , na inatarajiwa kuondoka kesho Ijumaa kuelekea Mkoani Dodoma.

Timu ya Kilombero, itasafiri hadi mji wa  mpwapwa ili kupambana na Timu ya Mpwapwa mji mechi itakayochezwa siku ya Jumamosi  November 30 katika Uwanja wa Mji Mpwapwa uliopo wilayani humo.

Mwenyekiti wa Kilombero Soka Net Academy  Mohamedi Kambi akizungumza na Michuzi Blog, amesema kuwa maandalizi yote yamekamili na wapo tayari kupambana na Mpwapwa Mji kwani kikosi chao kimejiandaa kwa ajili ya kupata ushindi.


Ameongeza amesema kuwa Mwalimu amewandaa vyema wachezaje wake kucheza mchezo huo wa ugenini na amewahakikishia wana Kilombero kuwa watarudi na ushidi mnono kutoka kwa wana Mpwapwa hiyo sikU hivyo wasiwe na shaka kabisa.

Katika hatua nyingine amewaomba watanzania hususani Wanamorogoro kwa ujumla kuichangia timu hiyo kwani ni mara ya kwanza inacheza michuano hiyo na inavijana chipukizi wanaohitaji kuendelezwa kwenye timu hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad