ONGEZEKO LA WATALII NI CHACHU YA UKUAJI WA SEKTA YA UTALII NCHINI-KIGWANGALA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 21 November 2019

ONGEZEKO LA WATALII NI CHACHU YA UKUAJI WA SEKTA YA UTALII NCHINI-KIGWANGALA

* Amewataka bodi ya utalii kutumia fedha zao na za wadau kuutangaza utalii 

*Awapongeza kwa kuingia makubaliano na Kampuni ya NAS kwa ajili ya kutangaza vivutio vya utalii..

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamis Kigwangala amesema idadi ya watalii imekuwa ikiongezeka na kuonesha dalili nzuri ya ukuaji wa sekta hiyo nchini.

Hayo ameyasema leo wakati wa uzinduzi wa Ushirikiano wa kutangaza utalii kati ya bodi ya Utalii (TTB) na Kampuni ya National Aviation Services (NAS) leo.

 Kigwangala amesema usafiri wa anga ni kichocheo kikubwa kwa ukuaji wa sekta ya utalii kwani watalii wengi kutoka nje ya nchi hutumia usafiri wa anga na takribani kwa mwaka 2028 watalii 929,022 (62%) walitumia anga, na 563,088 (37%) walitumia usafiri wa barabara na  13,592 ( 0.1%) walitumia reli na maji.

"Kumekuwa na ongezeko la watalii ambaopo kwa mwaka 2018 idadi imeongezeka na kufikia 1,505,702 tofauti na  watalii wailofika mwaka 2017 walikuwa ni 1,327,143 na mapato yakiwa ni dola za Kimarekani bilion 2.2 na kupanda hadi 2.4 2018," amesema Kigwangala.

Amesema, moja ya sekta mhimili mkuu wa uchumi ni utalii kwa asilimia 17,  na ni sekta inayoongoza katika kuchangua maendeleo ya uchumi nchini kwa kutoa ajira sawa  a aslimia 11.

Kigwangala amezitaka TTB na NAS kushirikiana kwa pamoja kuvitangaza vivutio vya utalii nchini ili kuzidi kuvutia watalii kutoka nchi mbalimbali, pia kutoa matangazo yatakayoonesha vivutio hivyo.

Mwenyekiti wa Bodi wa TTB Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amesema makubaliano yao na NAS ni miongoni mwa mbinu mpya za bodi hiyo katika kuendeleza kutangaza vivutio vya utalii nchini pamoja na kuitangaza Tanzania kama kituo bora cha utalii.

"Miongoni mwa masoko ambayo TTB kwa sasa tumeweka msukumu mkubwa sana katika kujitangaza kwa lengo la kuyafungua masoko ni katika nchi zilizoko mashariki ya kati na bara la Asia kwa ujumla ambapo kampuni ya NAS inatoa huduma kwenye Viwanja vya ndege," amesema Mihayo.

"Jukumu la TTB ni kutangaza vivutio vyote vya utaluu vinavyopatikana nchini Tanzania na pia kuitangaza Tanzania , kutafuta masoko ya utaliu nje ya nchi na kuwasahawishi watalii kutoka nchi hizo kuja kutembelea na kujionea vivutio vyetu,"amesema.


Naye Mjumbe wa Bodi ya NAS Afrika Balozi Prof Costa Mahalu ameeleza kuwa kampuni yao inahusika na utoaji wa huduma kwa abiria, ndege na mizigo ikiwemo vyumba vya kusubiria ndege yaanu VIP Lounges na CIP Lounges zaidi ya 40 katika nchi mbalimbali.

Mahalu amesema, kwa sasa kampuni yao inatoa huduma katika viwanja 40 vya ndege katika nchi 17 za Afrika, Mashariki ya kati na Asia  na inahudumia zaidi ya ndege 100 za makampuni mbalimbali ya ndege

"Kampuni inaendelea kuwekeza nchini Tanzania na mpaka sasa tumewekeza kiasi cha Shiling bilion 25 na itaendelea kuwekeza zaidi katika nchi za Afrika ikiwemo Tanzania kiasi cha bilion 100 kwani ni nchi inayofaa kuendelea kuwekeza kutokana na mazingira mazuri ya kibiashara, amani na utulivu," Mahalu amesema.

Ameongezea kwa nchini Tanzania, NAS wanahudumia katika viwanja vya Julius Kambarage Nyerere na KIA kilimanjaro.

TTB na NAS wameingia makubaliano hayo kwa kusaini mkataba utakaowawezesha kufanya kazi kwa pamoja katika kuitangaza nchi na vivutio vyake.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamis Kigwangala akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ushirikiano wa kutangaza utalii kati ya bodi ya Utalii (TTB) na Kampuni ya National Aviation Services (NAS) leo.
Mjumbe wa Bodi ya NAS Afrika Balozi Prof Costa Mahalu akizungumzia faida ya ushirikiano wao na bodi ya utalij katika kuutangaza utalii nchini. Uzinduzi wa Ushirikiano wa kutangaza utalii kati ya bodi ya Utalii (TTB) na Kampuni ya Nationa Aviation Services (NAS) leo.
Mwenyekiti wa Bodi wa TTB Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akizungumzia makubaliano yao na NAS ni miongoni mwa mbinu mpya za bodi hiyo katika kuendeleza kutangaza vivutio vya utalii nchini pamoja na kuitangaza Tanzania kama kituo bora cha utalii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii TTB Devota Mdachi na Mjumbe wa Bodi ya NAS Afrika Balozi Prof Costa Mahalu  
Wakitiliana saini makubaliano ya ushirikiano wa kutangaza utalii kati ya bodi ya Utalii (TTB) na Kampuni ya National Aviation Services (NAS)  katika Vyumba vya kusubiri VIP na CIP Lounges 40 na katika nchi 17 Afrika, Mashariki ya Kati na Asia. Chini wakionesha mkataba huo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamis Kigwangala (katikati),  Mwenyekiti wa Bodi TTB Jaji Mstaafu Thomas Mihayo (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa TTB Devota Mdachi (wa pili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa NAS Miguel Serea (kushoto) na Mjumbe wa Bodi ya NAS Afrika Balozi Prof Costa Mahalu  wakiwa katika picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad