HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, November 16, 2019

DAWASA FC YAENDELELA KUFANYA VIZURI LIGI YA MASHIRIKA


Timu ya mchezo wa Mpira wa miguu ya Mamlaka ya Majisafi nan Usafi wa Mazingira Dar esSalaam (DAWASA) imeendelea kuibuka kidedea katika ligi inayoendelea ya mashirika mballimbali yakijumuisha Umma, binafsi ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa timu hiyo, Mhandisi Boniface Philemon amesema ligi hiyo inayoendelea kupigwa  katika viwanja vya Gymkhana,   DAWASA FC waliweza kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya  Global Publishers FC.

Philemon ameeleza kwa sasa timu hiyo inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa tayari na alama 7 tangu mzunguko wa ligi uanze.

“DAWASA FC tumekuwa vinara katika mechi nyingi tulizoshiriki katika ligi hii kwa kuwa wachezaji wetu wamejituma hivyo tunategemea kuondoka na kombe mwisho wa ligi”

Aidha Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA FC Bakari Makilagi amewaasa mashabiki wa timu hiyo kujitokeza na kushiriki katika mechi zinazoendelea katika ligi hiyo ili waweze kuwashangalia na kuongeza morali kwa wachezaji.

Amesema, kuja kwao kwa wingi kutaifanya timu yao kufanya vizuri katika michuano hiyo.

Timu ya DAWASA FC inawachezaji 54 waliosajiliwa lakini katika ligi hiyo wameshiriki wachezaji 22 ambapo kuna vikosi viwili na kila kikosi kina jumla ya wachezaji 11.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad