HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 4, 2019

SHIRIKA LA SMILE TRAIN YAKABIDHI MASHINE ZA OPERESHENI YA MDOMO WAZI CCBRT

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Smile Train limetoa msaada wa mashine za kufanyia operesheni kwaajili ya kuwatibu watoto wanaozaliwa wakiwa na mdomo (Mdomo Sungura)katika Hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kurejesha furaha kwa watoto hao.

Mkurugenzi wa Smile Train Afrika Mashariki Jane Ngige amesema leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wazazi wa watoto waliozaliwa na mdomo wazi (Mdomo Sungura) wakati akitoa mashine hizo.

Ngige amesema kuwa watoto wanatakiwa kuhudhuria shuleni bila kutengwa wala kuchekwa kwasababu tu ya kuzaliwa na tatizo la mdomo wazi, hivyo mashine ambazo wamezitoa kwa hospitali hiyo zitasaidia kufanya operesheni kwa watoto na hatimaye kurejesha furaha na kutobaguliwa na wenzao.

"Habari njema ni kwamba hali hii inaweza kuondolewa kwa kufanyiwa operesheni ya kawaida tu na wengine huenda wakafanyiwa operesheni zaidi ya mara moja, hivyo Smile Train tutaendelea kuiunga mkono CCBRT kwa kuwapa furaha maelfu ya watoto wanaozaliwa na tatizo la mdomo wazi,"amesema.

Kwa upande wake Dk.Zainau Ilonga kutoka CCBRT ameeleza tatizo la mdomo wazi linavyokuwa ambapo amefafanua mtoto mwenye tatizo hilo anazaliwa akiwa na uwazi kwenye sehemu ya juu ya mdomo au ya chini.

Amesema sababu za tatizo hilo huwa linatokea pale mtoto akiwa tumboni, sehemu ya mdomo juu au chini zinashindwa kuungana."Ni rahisi mtoto kuzaliwa akiwa na mdomo wazi wa chini au juu au yote miwili, na hili tatizo lipo katika nchi nyingi duniani ambapo kila watoto 500 hadi 700 mmoja anazaliwa na mdomo wazi lakini inategemea na eneo na shughuli za kiuchumi ndani yenyewe,"amesema.

 Dk. Ilonga amesema kwa Tanzania watoto wasiopungua 2500 wanazaliwa na mdomo wazi na sababu zake kwa hapa nchini haijafahamika lakini kuna sababu mbalimbali ambazo zinachangia mtoto kuzaliwa akiwa na mdomo wazi.

Ametaja baadhi ya sababu hizo ni uvutaji sigara kwa mama mjazito, uzito kupita kiasi na wakati huo huo zipo sababu zinazotokana na utumiaji wa dawa.

Awali Ofisa Rasilimali Watu na Maendeleo wa CCBRT Anastazia Melis amesisitiza kuwa kwa watoto wanaozaliwa na mdomo wazi wanapopata huduma ya operesheni ya kuondoa tatizo hilo wanakuwa na amani ya moyo kwani hawatakuwa kuwa katika kundi la kuchekwa au kubaguliwa.

Pia ametumia nafasi hiyo kuwashukuru Smile Train kwa kusaidia mashine 3259 ndani ya miaka saba. Pia amewaasa wananchi kwa ujumla wenye midomo wazi wwaende latika hospitali ya CCBRT wakafanyiwe Operesheni kwani huduma hiyo ni bure kabisa.
 Mkurugenzi wa shirika la Smile Train's Afrika Mashariki,  Jane Ngige(Katikati) akizungumza na waandishi wa habari juu ya siku ya maadhimisho ya siku ya furaha ambayo hufanyika kila ifikapo Oktoba 5 kila mwaka.
Katika Kusheherekea siku hii shirika la Smile Train's wametoa mchango wa mashine za kufanyia upasuaji watoto wanaozaliwa na mdomo wazi katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam leo ili kushiriki furaha na watu wote bila kuwatenga watu katika siku mhimu kama siku ya furaha.
 Kushoto Daktari wa upasuaji wa hospitali ya CCBRT, Zainab Ilonga akizungu na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa maadhimisho ya siku ya furaha ambayo hufanyika kila ifikapo Oktoba 5 kila mwaka ili kushiriki furaha na watoto pamoja na watu wazima waliozaliwa na mdomo wazi na kufanyiwa oparesheni ili kuondoa hali ya kuwa na mdomo wazi. Na kulia ni Mkurugenzi shirika lisilo la kiserikali Afrika Mashariki wa shirika la Smile Train's, Jane Ngige
 Mmoja wa mzazi ambaye mtoto wake alizaliwa na mdomo wazi na akafanyiwa upasuaji katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa habari jinsi mtoto wake alivyotibiwa katika hospitali hiyo bila gharama zozote.
 Baadhi ya wazazi wa mzazi wa mtoto mwenye mdomo wazi, Veronika Joseph akizungumza na waandishi wa habari wakati akisubiria matibabu ya mtoto wake aliyezaliwa na mdomo wazi. Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amesema kuwa jamii kwa ujumla ijue kuwa matibabu ya watoto wanaozaliwa na mdomo wazi waende katika Hospitari ya CCBRT jijini Dar es Salaam kwani matibabu ni bure.
Pia amesema kuwa jamii kwa ujumla ionapo mtoto mwenye mdomo wazi wasimnyanyapae kwani hiyo hali watoto huzaliwa nayo.
Ofisa wa maliasili watu na maendeleo wa hospitali ya CCBRT, Anastansia Melis akikabidhiwa mashine ya kufanyia upasuaji kwa watoto waliozaliwa na mdomo wazi kutoka Mkurugenzi wa Afrika Mashariki wa shirika la Smile Train's, Jane Ngige katikati ni Daktari wa upasuaji wa hospitali ya CCBRT, Zainab Ilonga. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad