KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YATEMBELEA BANDARI YA DAR ES SALAAM - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 23 October 2019

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YATEMBELEA BANDARI YA DAR ES SALAAM

KAMATI ya kudumu ya Bunge ya Bajeti leo Oktoba 23 imetembelea Bandari ya Dar es Salaam na kujionea namna shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka ya Bandari hiyo.


Kamati hiyo imeshuhudia namna upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam unavyoendelea pamoja na kuona shughuli mbalimbali za uendeshaji wa bandari hizo unavyoendelea, katika ziara hiyo kamati hiyo iliambatana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwele.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe akitolea ufafanuzi kuhusu upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam pamoja na kuweka reli kwa ajili ya kusafirisha mizigo moja kwa moja mara baada ya kupakuliwa kutoka kwenye meli za Mizigo zinazofika Bandarini hapo wakati wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti ilipotembelea bandari hiyo leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Deusdedit Kakoko akionesha gati namba moja iliyojengwa hivi karibuni kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa bandari hiyo pamoja na kupungumza msongamano wa meli zinazofika kwenye bandari ya Dar es Salaam wakati wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti  ilipotembelea bandari hiyo leo.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Adadi Rajabu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kamati hiyo kutembelea bandari ya Dar es Salaam ili kuona ufanyaji wa kazi kwenye bandari hiyo leo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kutembelea bandari ya Dar es Salaam leo na kujione ufanisi mkubwa wa bandari hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad