HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 11 October 2019

Benki ya CRDB Tawi la Holland yaadhimisha wiki ya huduma kwa wateja

Benki ya CRDB Tawi la Holland wameadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati katika kuwahudumia wateja wao katika hilo.

Maadhimisho hayo ni katika kuhakikisha wiki ya huduma kwa wateja inaenda sambamba na kuwasogeza idadi ya wateja kufungua akaunti mbalimbali katika benki ya CRDB.

Wiki ya huduma kwa wateja imeanza Oktoba 7 na Kumalizika Oktoba 11 na maadhimisho yake ni kila mwanzoni mwa mwezi Oktoba kila mwaka.


Benki ya CRDB Tawi la Holland imekuwa na utaratibu wa kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kila mwaka na mafanikio yamekuwa yanaonekana kwa idadi ya wateja kufungua akaunti katika benki hiyo.

Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Holland, John Almas akizungumzia muitikio wa wateja kwenye wiki ya huduma kwa wateja katika tawi hilo lililopo jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha maadhimisho hayo yaliyoanza Oktoba 7 na kumalizika leo Oktoba 11, 2019 na maadhimisho yake ni kila mwanzoni mwa mwezi Oktoba kila mwaka.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB Tawi la Holland jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye picha za pamoja wameshika vipeperushi vya benki hiyo wakati wa wakati wa kilele cha maadhimisho hayo yaliyoanza Oktoba 7 na kumalizika leo Oktoba 11, 2019.
 Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Holland, John Almas akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo leo asubuhi wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja iliyoanza Oktoba 7 na kumalizika leo Oktoba 11, 2019.
No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad