HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 15, 2019

AFISA TARAFA ITISO AKATAA TAARIFA YA KAMATI YA MAJI, AAGIZA IANDIKWE UPYA

AFISA Tarafa wa Itiso, wa wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Remidius Emmanuel amewahamasisha wananchi  wa tarafa hiyo kuendelea kujiandikisha katika orodha ya Daftari la Wapiga kura kwa  kutambua thamani yaa kuchagua viongozi wa Kijiji na Kitongoji chao katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novenba  24 mwaka .

Afisa Tarafa huyo ameyasema hayo wakati akiwa katika ziarani katika  Kitongoji cha Wali (Kijiji cha Izava) kwa lengo la kuhamasisha wananchi hao kuendelea kujiandikisha katika orodha ya Daftari la Wapiga kura, ameesema kuwa  serikali inapanga maendeleo yake kuanzi ngazi ya mtaa, Kijtongoji  pamoja na Kijiji.

"Nyinyi ni mashahidi, wengi tumeshuhudia na kusikia Oktoba 12 mwaka huu  katika ardhi hii ya Wilaya ya Chamwino Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Pombe Joseph Magufuli alijiandikisha katika Kituo cha Sokoine (Chamwino Ikulu), Mheshimiwa Mkuu Wa wilaya yetu nae ameisha jiandikisha,mimi Afisa Tarafa wenu tayari nimejiandikisha, Sasa ni zamu yenu kujiandikisha kwa wingi wale ambao hawajashiriki zoezi hili.amesema Afisa Tarafa huyo.

 Katika hatua nyingine Afisa Tarafa  huyo ameikataa taarifa ya Mapato na Matumizi ya Kijiji cha Izava  iliyosomwa mbele yake baada ya wananchi kulalamika kwa  kipindi kirefu pasipo kusomewa mapato na Matumizi ya mradi wa Maji Kitongojini  hapo baada ya Afisa huyo kuwataka wananchi  waseme kero  zote zinazowakabili. 

Emmanuel amesema kuwa viongozi tunapaswa kuwajibika na kutendea haki nafasi na nyadhifa tulizo nazo, mambo haya ya kushindwa kusoma taarifa za mapato na matumizi ni tafsiri ya baadhi yetu kushindwa kutimiza wajibu wetu na kuwafanya wananchi kupunguza imani na viongozi wao.

Amesema wananchi wachague viongozi ambao watakuwa wanasoma mapato na matumizi kwa wakati  na kuweza kufanyika maendeleo kutokana na miradi  inayoendelea.
Hata hivyo Afisa tarafa huyo alikataa kuipokea taarifa iliyosomwa mbele yake na kamati hiyo  na kuagiza iandaliwe taarifa nyingine  itakayotoa mchanganuo sahihi pamoja na nyaraka muhimu ili wananchi hao waweze kusomewa taarifa sahihi ya mradi huo.

" Mfano,nimesikia kuna mahala hapa taarifa inaonyesha kwamba wajumbe walienda  kufungua akauti ya Maji  Dodoma na walitumia Tsh.400,000/=, Yaani kwenda Dodoma  na kufungua akauti mnatumia kiasi hiki cha fedha ?..Sasa nataka iandaliwe taarifa nyingine na iwe na mchanganuo wa mapato na matumizi ya fedha hizi ili wananchi wafahamu na lazima muweke na nyaraka zitakazoonyesha uhalisia wa matumizi hayo"  Amesema Afisa Tarafa.

Kwa upande wake  mwenyekiti wa kamati ya Maji  Amosi Mainaa Lugumbau aliwaomba radhi wananchi hao baada ya  kukiuka  makubaliano ya awali na kushindwa kuwasilisha taarifa za mapato na matumizi kwa wananchi wa kitongoji hicho pamoja na kutohusisha uongozi wa kijiji katika shughuli zote za mradi huo.

Katika ziara yake, Afisa Tarafa aliambatana na Mtendaji wa kata ya Segala Bi.Twahia komba pamoja na viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Izava.

 Afisa Tarafa Itiso Remidius Emmanuel akionyesha Stakabadhi ya Shilingi Milioni Moja iliyorejeshwa katika akaunti ya maji baada ya kamati ya maji kushikilia fedha hiyo kinyume na taratibu.

 Juma Mohamedi Moja ya wananchi wa Kitongoji cha Wali akiwasilisha kero yake kwa Afisa Tarafa -Itiso  Remidius Emmanuel katika mkutano huo.
 Mwananchi wa Kitongoji cha Wali Emmanuel Panga akisoma taarifa ya Mapato na Matumizi kwa niaba ya kamati ya Maji.Taarifa ambayo hata hivyo haikupokelewa na Afisa Tarafa. 

 Baadhi ya wananchi wa Kitongoji cha Wali walioshiriki Mkutano huo.
 Afisa Tarafa Itiso Remidius Emmanuel  akiwa na viongozi wa ngazi ya Kata, Kijiji na  Kitongoji husika

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad