Wahitimu wa JKT watakiwa kujiepusha na rushwa - DC Kilolo - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 5 September 2019

Wahitimu wa JKT watakiwa kujiepusha na rushwa - DC Kilolo

Vijana waliohitimu Mafunzo ya JKT kundi la Mujibu wa Sheria Operesheni Makao Makuu Dodoma wametakiwa kuikemea na kujiepusha na tabia za rushwa katika jamii.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asiyah Abdallah aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa kufunga mafunzo ya JKT kwa vijana wa Mujibu wa Sheria Operesheni Makao Makuu Dodoma Kambi ya Mafinga JKT mkoani Iringa.

"Rushwa ni adui wa haki, ni vyema mkaonesha kwa vitendo namna ya  kukemea na kujiepusha na matendo ya rushwa ndani ya  jamii yetu" amesema  Asiyah.

Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Kanali Hassan Mabena amewataka wahitimu hao kuyatumia mafunzo ya ulinzi waliyojifunza kusaidia jamii inayowazunguka na kamwe wasiyatumie mafunzo hayo katika kuwanyanyasa wananchi.

Ameongeza kwa kusema kuwa jamii ingependa kuona kwa vitendo namna vijana watakavyokuwa msaada mkubwa kwenye masuala mbalimbali yakiwemo ya  kiulinzi na usalama.

Mapema akisoma taarifa fupi ya kozi hiyo, Kamanda Kikosi cha Mafinga JKT, Luteni Kanali Issa Chalamila amesema kuwa mafunzo hayo yaliyofunguliwa  tarehe 17 Jun 2019 yakiwa na vijana 1514 yamechukuwa muda wa miezi mitatu ambapo vijana 15 walikosa uzalendo na uvumilivu na   kujikuta wanakimbia mafunzo hayo ya JKT.
Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asiyah Abdallah akimtunuku cheti mmoja wa waliohitimu Mafunzo ya JKT kundi la Mujibu wa Sheria Operesheni Makao Makuu Dodoma, yaliyofanyika leo katika Kambi ya Mafinga JKT mkoani Iringa.
 Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asiyah Abdallah akikagua paredi ya waliohitimu Mafunzo ya JKT kundi la Mujibu wa Sheria Operesheni Makao Makuu Dodoma, yaliyofanyika leo katika Kambi ya Mafinga JKT mkoani Iringa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad