TMA kutatoa utabiri wake wa msimu wa Mvua za Vuli kwa kipindi cha Oktoba, Novemba hadi Disemba - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 2 September 2019

TMA kutatoa utabiri wake wa msimu wa Mvua za Vuli kwa kipindi cha Oktoba, Novemba hadi Disemba

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Dk. Agnes  Kijazi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu utabiri wa mvua za vuli,  Octoba hadi Desemba (OND) unatarajiwa kutangazwa kesho mara baada ya kufungua semina ya wanahabari inayofanyika leo Septemba 2, 2019 kwenye makao makuu ya Mamlaka ya Hali ya hewa (TMA) Ubungo Plaza jijini Dar es salaam .
 Mchambuzi wa utabiri wa hali Hali ya Hewa nchini, kutoka TMA Abubakari Lungo, akiwaeleza waandishi wa Habari namna  utabiri unavyofanyika wakati wa warsha ya siku moja ya mundelezo wa taarifa ya hali ya hewa juu ya utabiri mvua za vuli, iliyofanyika leo Sepemba 2,2019 katika Makao Makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA, Ubungo jijini Dar es Salaam
 Mkurugenzi wa Huduma za utabiri, Hamza Kabelwa, akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari juu ya utabiri wa mvua za vuli unaotarajiwa kutangazwa kesho, pembeni yake ni ameneja wa huduma za utabiri Samwel Mbuya.

Na Karama Kenyunko,  Michuzi TV,

MAMLAKA  ya Hali ya Hewa nchini (TMA), kesho Septemba 3, 2019 itatoa utabiri wake wa msimu wa Mvua za Vuli kwa kipindi cha Oktoba, Novemba hadi  Disemba mwaka huu.

 Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi amesema hayo leo wakati akifungua warsha ya siku moja kwa waandishi wa Habari iliyofanyika katika Makao Makuu ya TMA, Ubungo jijini Dar ea Salaam.

 Amesema, kwa kuzingatia umuhimu wa taarufa za hali ya hewa, mamlaka  haina budi kutoa taarifa zake mapema na kwa wakati ili ziweze kufikia wananchi wote na sekta husika kwa ajili ya kuwawezesha kuchukua hatua stahiki ikiwemo kuepukana na majanga yanayoweza kusababishwa na mvua kwa kuwa matumizi ya taarifa za hali ya hewa kwa jamii katika shughuli zetu za kila sik ni ya muhimu.

Amesema, TMA, imekuwa ikahakikisha inakutana na wanahabari ambao ni daraja muhimu kati ya taasisi zetu za serikali na wananchi wote kwa ujumla katika kuwapa warsha mbali mbali za kujadili mwelekeo wa msimu wa Mvua na kuongeza kuwa Serikali ya Awamu ya tano inatambua vyema mchango wa huduma za hali ya hewa nchini na umuhimu wa kuwafikia wananchi kwa wakati.

Dkt, Kijazi Amesema, lengo la warsha ya lei ni kujadili Mwelekeo wa Msimu wa Mvua za vuli kwa kipindi cha Oktoba hadi Disemba mwaka huu na kujadili athari zinazoweza kujitokeza, hivyo wataalamu wameandaa rasimu ya mwelekeo huo na viashiria vilivyopelekea kupatikana kwa utabiri huu, Aidha amesema kutokana na maoni ya wanahabari na wadau wengine kuhusu lugha inayotumika kuwasilisha taarifa za hali ya hewa.

Mamlaka kwa kushirikiana na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na taasisi zingine ikiwemo BAKIZA na vyuo vikuu, imeweza kutafsiri baadhi ya maneno kwa lugha ya Kiswahili hivyo kupitia warsha hiyo wanahabari wamepata fursa ya kuona baadhi ya misamiati ya hali ya hewa iliyo katika lugha ya Kiswahili kwa lengo la kutoa maoni kabla haijaanza kutumika rasmi.

"Lugha ya kiswahili itasaidia wananchi kwa wingi, kuelewa utabiri wa hali ya hewa pale unaposomwa kwabi wakati mwingine imesheheni maneno ya kisayansi na yasiyo rahisi kueleweka na jamii,," amesema Dkt.kijazi

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad