Tigo yazindua huduma ya kwanza na ya kipekee ya Home Internet - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 3 September 2019

Tigo yazindua huduma ya kwanza na ya kipekee ya Home Internet

Wateja wa Kampuni ya mawasiliano,Tigo, kwa mara ya kwanza watapata fursa ya kufurahia huduma Home Internet yenye kasi ya 4G+ majumbani mwao. Huduma hii ni ya kwanza na ya kipekee Tanzania, yenye ubunifu wa hali ya juu itakayowafanya wateja wafurahie intaneti ya 4G+ kwa kutumia vifaa vya Router au Modem.

Kampuni ya simu ya Tigo imezindua rasmi huduma hiyo ambayo itatatua changamoto ambazo watumiaji wa mitandao ya simu hususan wale wa majumbani wamekuwa wakikabiliana nazo.

Kupitia huduma hiyo, wateja wa kampuni ya Tigo sasa watapata fursa ya kupanga na kuchagua ni jinsi gani watatumia huduma ya intaneti, ikiwemo kununua vifurushi, kuongeza na kuangalia salio kupitia simu zao za mkononi.

“Mrejesho kutoka kwa wateja wetu umeonyesha kwamba kuna umuhimu wa uwepo wa huduma rahisi na ya uhakika ya mtandao wa intaneti majumbani. Hata hivyo, uzoefu katika matumizi ya huduma ya mtandao wa intaneti majumbani kwa wateja ni jambo lenye umuhimu mkubwa sana kwetu,” ameeleza Mkuu wa kitengo cha Biashara cha Kampuni ya Tigo, Tarik Boudiaf.

“Zama zile za mteja kusumbuka kutumia simu yake ya mkononi kama modem au kuhamisha line inayotumika kwenye modem au router ili kupata huduma ya intanet zimekwisha pita kitambo. Zama za kununua kifurushi ama kuongeza au kuangalia salio la laini inayotumika kwenye modem au router kwa kutumia kifaa kingine, ni jambo ambalo humpa mteja usumbufu, nazo zimekwisha pita kitambo,” ameongeza Boudiaf.

Kupitia huduma hii iliyozinduliwa na Tigo, wateja sasa wanaweza kupangilia matumizi yao ya huduma ya intaneti kwa kuunganisha vifaa vya modem na router kutumia Tigo Pesa App.

“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa kila mteja wa Tigo nchini ambaye atahitaji kutumia huduma yetu ya Home Internet anaunganishwa muda wote bila vikwazo vyovyote,” ameongeza Boudiaf.
Kwa mujibu wa Boudiaf, huduma hii mpya iliyozinduliwa kwa mara ya kwanza nchini ni sehemu tu ya jitihada za kampuni ya Tigo ya kutoa huduma zinazojali maslahi ya wateja katika kuwapa uzoefu endelevu wa kijiditali kupitia mtandao wenye kasi zaidi wa 4G+.

Uzinduzi wa huduma hii mpya umeshuhudiwa pia na Meneja huduma za intaneti wa kampuni ya Tigo, Mkumbo Myonga, ambaye amewahakikishia wateja kupata huduma bora na rahisi wanapojuanga na huduma ya Home Internet.

Ili kujiunga na kufurahia huduma hiyo ya Home Internet, wateja wa Tigo wanaweza kununua modem au router katika maduka ya Tigo yaliyopo nchi nzima. Wateja wa Home internet wanaweza kuwasiliana na kitengo cha huduma kwa wateja wakati wowote, yani masaa 24 kwa siku.

Ili kufurahia huduma hiyo, wateja wa kampuni ya mawasiliano Tigo wanaweza kununua kwa urahisi vifurushi vya Home Internet kwa kutumia Tigo Pesa App, au kwa kutembelea tovuti ya; internet.tigo.co.tzau pia kwa kupiga *147*00# ili kujiunga mwenyewe au kununulia ndugu, jamaa na marafiki kifurushi cha Home Internet.

Wateja wa Tigo watapata huduma hiyo ya Home Internet kulingana na thamani ya fedha zao kwa kununua kifurushi cha wiki au mwezi, kwa kuanzia Tsh15,000 kwa GB12 kwa siku 7 hadi Tshs120,000 kwa GB200 kwa mwezi mmoja.

Vifaa hivyo vitapatikana kwa urahisi kwa bei ya rejareja ya Sh150,000 kwa Modem na Sh250,000 kwa Routers, ambapo mteja wa Tigo akinunua atapata na kifurushi cha bure cha intaneti cha mwezi mmoja cha GB40 na GB100.
Meneja Huduma za Intaneti Mkumbo Myonga akiwaelezea waandishi wa habari,jinsi gani Mteja anaweza kuangalia salio, kununua kifurushi kwa kupitia Tigo Pesa App katika uzinduzi wa huduma ya kipekee ya Home Internet, Kushoto kwake ni Afisa Mkuu wa Biashara, Tarik Boudiaf.
Mkuu wa Bidhaa na Huduma kutoka Tigo, David Umoh akimkabidhi Home Internet Router Mtangazaji wa Clouds Tv, Abdallah Kamelo, katika uzinduzi wa huduma ya kwanza na ya kipekee ya Home Internet kutoka Tigo, Katikati ni Afisa Mkuu wa Biashara, Tarik Boudiaf

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad