HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 16, 2019

NAIBU WAZIRI KANYASU AWAFUNDA WAZAZI WENYE WATOTO WALIOHITIMU DARASA LA SABA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Geita mjini, Mhe.Constantine Kanyasu amewahimiza wazazi wenye watoto waliomaliza darasa la saba mwezi huu nchini  wahakikishe wanawalinda watoto hao wasijiingize katika makundi yasiyofaa.

Akizungumza kwenye mahafali ya saba ya wanafunzi 69 waliomaliza darasa la saba katika shule ya msingi ya Waja Springs ya mkoani Geita,Mhe.Kanyasu amewataka wazazi wawe mstari wa mbele katika malezi bora ya watoto wao

.Aidha, Mhe.Kanyasu amewataka pia wahitimu hao wakawe mfano bora katika jamii kwa kuwa kuwasaidia wazazi wao kwa kufanya kazi za majumbani badala ya kuacha kazi zote zifanywe na Wafanyakazi wa ndani

Katika hatua nyingine, Mhe. Kanyasu ameipongeza shule hiyo kwa kufanya vizuri katika mitihani ya Taifa na  kuufanya mkoa wa Geita kuwa miongoni mwa  mkoa inayokuwepo kwenye tano bora kitaifa.

Pia, Mhe.Kanyasu amewataka wanafunzi hao watumie muda mwingi kujisomea vitabu vya hadithi badala ya kutumia muda mwingi kuangalia Televisheni hasa vipindi visivyofaa

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu ameuhakikishia Uongozi wa shule hiyo kutafuta ufumbuzi wa tatizo la barabara iinayoelekea katika shule hiyo pamoja tatizo maji machafu wakati mvua ikinyesha . 

Kwa upande wake Meneja wa Shule hiyo, Mhandisi.Chacha Wambura amewaasa wazazi kujiepusha kuwapatia simu watoto wao ili wasiweze kuingia katika vishawishi katika kipindi hili kifupi walichohitimu masomo yao.

" Wazazi jiepusheni kuwapa simu zenu hawa watoto, hii mitandao ya kijamii inawapelekea watoto kuanza kuangalia mambo yasiyofaa " alisisitiza Wambura.

Aidha, Amewataka Wahitimu hao waache kuzitumia simu za wazazi wao pindi wakiwa majumbani badala yake wasome vitabu kama walivyokuwa wakifundishwa shuleni

Naye, Janeth Ndibalema ambaye ni mzazi wa mhitimu wa darasa la saba, Amesema malezi ya watoto kwa sasa yamekuwa na changamoto nyingi kutokana na wazazi kuacha jukumu la malezi kwa Wasichana wa kazi  hali  inatopelekea watoto wengi kuharibikiwa.

Kufuatia hali hiyo, Ndibalema ametoa wito kwa wazazi kutenga muda kukaa na watoto wao badala ya kujikita kwenye majukumu ya kazi ili kuwasaidia watoto wao kujiepusha kufanya mambo yasiyofaa yatakayowafanya wasiweze kuendelea na shule.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akimkabidhi cheti, Janeth Ibrahim miongoni mwa wanafunzi  aliyehitimu darasa la saba katika shule ya msingi ya Waja Springs wakati wa mahafali ya saba yaliyofanyika katika shule hiyo  iliyopo mkoani Geita.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akivishwa  skafu na  Sara Keneth ambaye ni wanafunzi wa darasa la sita  katika shule ya msingi ya Waja Springs wakati  Naibu Waziri huyo alipowasili katika shule hiyo akiwa mgeni rasmi katika mahafali  ya saba ya darasa la saba yaliyofanyika mkoani Geita.
 Wahitimu wa darasa la saba wa shule ya msingi ya WAJA Springs wakiwa pamoja na wanafunzi wenzao wakiimba wimbo wa taifa mara baada ya mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu kuwasili katika shule hiyo kwa ajili ya mahafali ya darasa la saba 
 Wanafunzi wa shule ya msingi ya Waja Springs wakiimba ikiwa ni ishara ya kuwaaga wenzao wahitimu wa darasa la saba katika mahafali yaliyofanyika katika shule hiyo mkoani Geita.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akimkabidhi zawadi mwanafunzi bora aliyekuwa akifanya vizuri kwenye masomo yake, Charles Zungu kwenye mahafali ya darasa la saba katika shule ya msingi ya Waja Springs iliyopo mkoani Geita.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi, wamiliki wa shule pamoja na wazazi wa wanafunzi waliohitimu darasa la saba katika mahafali ya saba ya katika shule ya msingi ya Waja Springs iliyopo mkoani Geita

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad