HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 26, 2019

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI TISA MBINGA MJI YA MILIONI 924

MWENGE wa uhuru umefungua, umepitia, umekagua, umezindua na kuweka jiwe la msingi la miradi tisa ya thamani ya shilingi 924,150,266.14 kwenye Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mkoani Ruvuma. 

Mkurugenzi wa mji wa Mbinga, Grace Quintine akizungumza jana wakati akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, Gipson Mhagama alisema mwenge huo umekimbizwa kwenye kilomita 118.

Quintine alisema katika mradi wa kwanza, mwenge huo wa uhuru utafungua nyumba bora ya mwananchi wa kijiji cha Mpepai. 

Alisema mwenge huo umefungua zahanati ya kijiji cha Lipilipili na kukagua shamba bora la miti ya hifadhi ya mazingira. 

Alisema utazindua klabu ya wapinga rushwa ya shule ya sekondari Depaul Mbangamao na kuweka jiwe la msingi shule ya sekondari Kagugu. 

"Utazindua mradi wa maji Maganagana, kuweka jiwe la msingi mtambo wa kumenya kahawa Sepukila na kufungua kiwanda cha maji Asili (Mdaka Five) mtaa wa Masumuni na kuweka jiwe la msingi barabara ya Mbuyula," alisema Quintine. 

Alisema baada ya kukimbizwa kwenye halmashauri ya mji wa Mbinga, mwenge wa uhuru utakabidhiwa katika halmashauri ya wilaya ya Songea. 

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa wa mwaka huu, Mzee Mkongea Ally aliipongeza halmashauri ya mji wa Mbinga kwa kuwa na miradi mizuri yenye tija kwa jamii.

"Katika mradi wa zahanati ya Lipilipili wananchi wanapaswa kutumia huduma za afya kuliko kujitibu kwa waganga wa kienyeji kwani ni muda mrefu hamkua na zahanati," alisema Ally.


Ally alisema mradi wa maji wa Asili wa Mdaka Five umeongeza ajira na barabara ya Mbuyula nayo imejengwa kwa kiwango kinachostahili.

Kauli mbiu ya mwenge wa uhuru kitaifa wa mwaka 2019 ni maji ni haki ya kila mtu, tutunze vyanzo vyake na tukumbuke kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa. 
 Mkurugenzi wa Mji wa Mbinga Mkoani Ruvuma, Grace Quintine akipokea mwenge wa uhuru kwa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Gipson Mhagama ambao ulizindua miradi tisa ya Halmashauri ya mji huo yenye thamani ya shilingi 924,150,266.
 Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka huu Mzee Mkongea Ally akipokewa na viongozi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mkoani Ruvuma.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka huu Mzee Mkongea Ally akizungumza baada ya kuzindua mradi wa zahanati ya Kijiji cha Lipilipili Halmashauri ya Mji wa Mbinga ambao awali wananchi wa eneo hilo walikuwa wanatembea umbali mrefu wa kilomita saba kufuata huduma ya afya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad