



Akifungua Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upataji Taarifa yaliyofanyika mkoani,Waziri wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Balozi Augustine Mahiga amesema; Haitoshi kusema haki iko katika katiba, Taarifa lazima ziwe kamili ziwe zinaielewa jamii yetu. Tuna chombo cha Lugha yetu ya Kiswahili tukitumie.
Washiriki wa maadhimisho hayo kutoka asasi na taasisi mbali mbali walipata fursa ya kushiriki majadiliano katika makundi ambapo walijadili masuala ya umuhimu wa upataji taarifa na kupata fursa ya kuwasilisha kwa pamoja na kuyajadili.
Washiriki Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upataji Taarifa wa katika makundi.
Wawasilishaji mada kwa niaba ya makundi wakifuatilia michango na maoni kutoka kwa washiriki wengine.
Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mheshimiwa Regina Chonjo akizungumza na washiriki maadhimisho.
Akifunga maadhimisho hayo, Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mheshimiwa Regina Chonjo aliwapongeza waandaji wa maadhimisho hayo na kusisitiza kuwa taarifa hizi ziwe za kweli na zenye tija kwa maendeleo binafsi,taasisi na taifa kwa ujumla.




Sambamba na hilo Mheshimiwa Regina aliwashukuru wadau kwa kuamua kufanyia maadhimisho hayo mkoani Morogoro na kutoa rai kwa taasisi nyingine kuiga mfano huu kwani jambo jema kuwekeza fursa za kiuchumi katika mikoa yote nchini badala ya kuzielekeza maeneo machache yaliyozoeleka.
Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mheshimiwa Regina Chonjo akipokea cheti cha pongezi za ushiriki wa maadhimisho hayo kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO nchini Nancy Kaizilege kwa niaba ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
Mkurugenzi wa MISA Tanzania Bw. Gasirigwa Sengiyumva akipokea cheti cha pongezi za ushiriki wa maadhimisho hayo kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mheshimiwa Regina Chonjo.
Matukio katika picha ,washiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upataji
Taarifa.







No comments:
Post a Comment