HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 9, 2019

DKT. KALEMANI "AKUNWA" NA KASI YA UJENZI MRADI WA UMEME WA MAJI WA JULIUS NYERERE (JNHPP) WA MTO RUFIJI

Ujenzi wa nguzo za daraja namba moja litakalounganisha pande mbili za mto Rufiji ukiwa unaendelea. Daraja hilo litasaidia kuvusha vifaa vya ujenzi (mashine) kutoka upande mmoja wa mto kwenda upande wa pili ili kusaidiana na daraja namba mbili ambalo tayari linafanya kazi.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

KASI ya ujenzi wa mradi wa umeme wa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) kwenye Mto Rufiji Mkoani Pwani “imemkuna” Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani baada ya kutembelea eneo la mradi huo Jumapili Septemba 8, 2019 na kukuta hatua muhimu ya ujenzi wa ADIT (njia ya kufika kwenye mifereji mikubwa ya kuchepusha maji) (diversion tunnel), pamoja na miundombinu wezeshi ikiwa imekamilika.

Sambamba na kupigwa kwa hatua hizo muhimu katika utekelezaji wa mradi huo uliozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Julai 26, 2019 na ambao utazalisha Megawati 2115, pia amepongeza usimamizi na utawala katika mradi huo.

“Hii ni mara yangu ya nane kutembeela mradi huu tangu uanze, leo nimetembelea ili kuangalia masuala makubwa matatu, kasi ya ujenzi, usimamizi na utawala na masuala yote ya ujenzi wa miundombinu wezeshi ili kuona kama imekaa sawasawa.” Alisema Dkt. Kalemani.

Alisema baada ya kuangalia masuala hayo amefurahishwa na hatua iliyofikiwa ambapo amewapongeza wasimamizi wa mradi huo TANESCO na TANROADS ambao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alitoa maelekezo kuwa lazima ujenzi huo usimamiwe na Watanzania wenyewe na ukamilike katika muda uliopangwa ambao ni miezi 42, ambapo miezi 36 ni ya ujenzi na miezi 6 ya mobilization kwa maana ya maandalizi ya vifaa na watumishi ambapo kazi ilianza Juni 15, 2019 na kazi inakwenda vizuri.” Alifafanmua Dkt. Kalemani.

Akifafanua zaidi Dkt. Kalemani alisema hadi sasa tayari wakandarasi wamekwishatumia miezi nane 8 kati ya 42 na kazi ambazpo zilikuwa zinaendelea kufanyika ni ujenzi wa njia za kuchepusha maji ardhini (diversion tunnel), nilikuja Julai 22, 2019 na nikaelekeza kazi hii ifanyike ndani ya siku 45 na ikamilike. ADIT hiyo yenye urefu wa wa Mita147.6 nashukuru wamemaliza na wameokoa siku 7 kabla ya muda niliotoa.

Mheshimiwa Dkt. Kalemani pia alisisitiza kuwa ni matumaini ya serikali kwamba wakandarasi watamaliza kazi ya ujenzi ndani ya muda na kwamba hakuna muda utakaoongezwa.
 
“Nimatarajio yetu mkataba unaisha Juni 14, 2022 na nimatumaini yetu pia watatukabidhi mradi huo siku hiyo saa 9;30 alasiri ili na mimi niukabidhi kwa Watanzania.” Alisisitiza na kuongeza…asitokee mtu atakaejaribu kuuchelewesha mradi huo, sisi kama serikali tutahakikisha tunaanza kumchelewesha yeye kwanza kabla hajatuchelewesha sisi kukamilisha mradi huo muhimu kwa taifa letu.” Alionya.
Alisema mradi huo wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPP) ni muhimu, bwawa hilo ni kubwa sana aliwataka Watanzania kutunza vyanzo vya maji yanayoelekea kwenye mto Rufiji ili kuwepo uhakika wa upatikanaji wa maji ya kutosha ni bwawa hili litahitaji maji kwenye ujazo wa mita za ujazo bilioni 33.2 hivyo maji ya kutosha yatahitajika.

"Bwawa hili ni kubwa kati ya mabwawa 70 duniani bwawa la JNHPP ni bwawa mojawapo, kati ya mabwawa manne makubwa Afrika bwawa hili ni mojawapo na ni la kwanza kwa ukubwa Afrika Mashariki kwa hivyo Watanzania wanayo kila sababu ya kujivunia na ni wajibu wetu kuyinza na kuhifadhi vyanzo vuya maji." Alisisitiza.

Alisema manufaa ya mradi huo ni pamoja na kuongeza umeme kwenye gridi ya taifa, kusambaza umeme vijijini na kwenye viwanda, pia utasaidia sana kupunguza uharibifu wa mazingira.

Awali akitoa taarifa ya mafanikio ya utekelezaji wa mradi huo yaliyofikiwa hadi sasa tangu uzinduliwe na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Mratibu wa Mradi huo Mhandisi Steven Manda ambaye pia ni Meneja Miradi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) alisema, pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa handaki la kuchepusha maji, pia daraja namba mbili kwa maana ya miundombinu wezeshi nalo limekamilika na sasa mashine kubwa na vifaa vya ujenzi vinavushwa kutoka upande mmoja wa mto kwenda upande wa pili kupitia daraja hilo.

WAZIRI wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, akitoa tathmini yake mbele ya sehemu ya kuingilia kwenye handaki la kuchepusha maji (diversion channel) la ujenzi wa mradi wa umeme wa maji wa Julius Nyerere kwenye mto Rufiji Mkoani Pwani leo Jumapili Septemba 8, 2019 wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo ambao ukikamilika utazalisha umeme wa Megawati 2115.

Daraja namba mbili la kukatisha mto Rufiji eneo la ujenzi wa mradi wa umeme wa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) likiwa limekamilika leo Jumapili Septemba 8, 2019.

Kijiko kikitoka kwenye handaki la kuchepusha maji leo Septemba 8, 2019.

Waziri Dkt. Kalemani akiwa na viongozi mbalimbali kwenye eneo la mradi.

Msafara wa magari ya Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani ukipita kwenye daraja namba mbili linalokatisha mto Rufiji leo Septemba 8, 2019.
Waziri Mhe. Dkt. Kalemani (katikati) akipatiwa maelezo na Mratibu wa mradi huo Mhandisi Steven Manda wakati wa ziara
Eneo la kuingilia ADIT (njia ya kufika kwenye handaki la kuchepusha maji) (diversion tunnel).
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Dkt. Kebwe Stephene Kebwe akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara hiyo.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Mheshimiwa Juma Abdallah Njwayo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara hiyo.
Dkt. Kalemani akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephene Kebwe na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Rufiji (OCD) Lepold Fungu, akipatiwa maelezo na Mmoja wa wasimamizi wa mradi huo.




Mhe. Dkt. Kalemani akimsikilzia Meneja Mradi kutoka kampuni ya Arab Contractor ya Misri, Mhandisi Mohammad Samaha.(kushoto).
Daraja namba mbili likiwa limekamilika na kufanya kazi
Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani akimsikiliza Mratibu wa ujenzi wa Mradi wa bwawa la kufua umeme la Nyerere (JNHPP), ambaye pia ni Meneja Miradi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Mhandisi Steven Manda, mara baada ya kutembelea maeneo kadhaa ya utekelezaji wa mradi huo Jumapili Septemba 8, 2019.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad