Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa'ichi akiongea kwa furaha na wanahabari mara baada ya kuruhusiwa kuondoka Taasisi ya Mifupa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MOI) alikokuwa akipatiwa matibabu kwa siku kadhaa. Wengine ni Askofu Msaidizi Eusebius Nzigilwa wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface (wa pili kushoto) na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Profesa Joseph Kahamba (kulia). Mhashama Askofu Mkuu Ruwa’ichi, ambaye alifikishwa hapo MOI akitokea katika Hospitali ya Rufaa Kilimanjaro (KCMC) Jumatatu Septemba 9 na kufanyiwa upasuaji mkubwa wa ubongo, amemshukuru Mungu kwa yote na pia amemshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kutoa msaada wa haraka wa ndege ya Rais kumsafirisha hadi Dar es salaam alikopatiwa matibabu Pia amewashukuru Madaktari wa KCMC kwa matibabu ya awali na wa MOI kwa kuokoa maisha yake kwa kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu. Vile vile amewashukuru waumini na Watanzania wote kwa ujumla kwa kumuombea.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mhashamu Yuda
Thadeus Ruwa'ichi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya madaktari
na wauguzi wa Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
MOI) pamoja na Askofu Msaidizi Eusebius Nzigilwa wa Jimbo Kuu
Katoliki la Dar es Salaam (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt
Respicious Boniface (wa pili kushoto) na Daktari Bingwa wa Upasuaji
wa Ubongo, Profesa Joseph Kahamba (kulia) baada ya kuruhusiwa kutoka
hospitali leo Jumatano Septemmba 25, 2019.
Mhashama Askofu Mkuu Ruwa’ichi, ambaye alifikishwa hapo MOI akitokea
katika Hospitali ya Rufaa Kilimanjaro (KCMC) Jumatatu Septemba 9 na
kufanyiwa upasuaji mkubwa wa ubongo, amemshukuru Mungu kwa yote na pia
amemshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kutoa msaada wa haraka wa
ndege ya Rais kumsafirisha hadi Dar es salaam alikopatiwa matibabu.
Pia amewashukuru Madaktari wa KCMC kwa matibabu ya awali na wa MOI kwa
kuokoa maisha yake kwa kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu. Vile
vile amewashukuru waumini na Watanzania wote kwa ujumla kwa kumuombea.
PICHA NA ISSA MICHUZI
No comments:
Post a Comment