UJUMBE WA BENKI YA DUNIA WAKUTANA NA MTENDAJI MKUU-MAHAKAMA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 28 August 2019

UJUMBE WA BENKI YA DUNIA WAKUTANA NA MTENDAJI MKUU-MAHAKAMA

Na Mary Gwera, Mahakama
Wataalamu kutoka Benki ya Dunia ‘World Bank’ wapo nchini kwa  lengo la kufanya tathmini ya maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama unaofadhiliwa kwa fedha za mkopo kutoka Benki  hiyo.

Lengo la Ujumbe huo kutembelea Mahakama ni kusaidia kukwamua vikwazo mbalimbali ili kuongeza kasi na ufanisi wa utekelezaji wa Mradi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Aidha; Wataalam hao ambao watakuwepo nchini kwa muda wa siku saba (7), waliwasili nchini  Agosti 23, 2019 na tayari wametembelea baadhi ya Miradi ya ujenzi ya Majengo ya Mahakama Kuu Musoma-Mara, Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu pamoja na kukagua maendeleo ya ufanyaji kazi ya Mahakama inayotembea ‘Mobile Court’ mkoani Mwanza.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Kitengo cha Maboresho cha Mahakama (JDU), Ujumbe huo pia tayari umekutana na baadhi ya Ofisi/Kurugenzi mfano Kurugenzi ya Ugavi na Ununuzi na vilevile Wajumbe hao watapatiwa taarifa za hatua  za utekelezaji wa malengo mbalimbali yaliyowekwa kwa kila Idara/Kitengo.

Hali kadhalika, Agosti 27, 2019, Ujumbe huo ulipata wasaa wa kukutana na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga na kufanya mazungumzo kuhusiana na utekelezaji wa Mradi huo.

Baada ya kukamilika kwa ratiba ya ugeni huo, watatoa maoni/mapendekezo ya maeneo ya kuyafanyia kazi zaidi ili kuboresha utekelezaji wa mradi huo wa miaka mitano (2015/2016-2019/2020).
 Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga akisalimiana na Bw. Denis Biseko, Mtaalam kutoka Benki ya Dunia-Tanzania pindi yeye pamoja na wenzake waliowasili ofisini kwa Mtendaji. Katikati ni Bi. Deborah Isser Mtaalam kutoka Benki ya Dunia-Washington-Marekani.

 Wajumbe kutoka Benki ya Dunia wakiwa ndani ya Mahakama inayotembea ‘mobile court’ iliyopo mkoani Mwanza, lengo ni kujionea hali ya ufanyaji kazi wa Mahakama hiyo.
  Picha ya pamoja baada ya mazungumzo; Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga (wa tano kushoto) katika picha ya pamoja na Wajumbe kutoka Benki ya Dunia na Mahakama, wa tano kulia ni Bi. Deborah Isser, Mtaalam kutoka Benki ya Dunia, wa nne kushoto ni Bw. Waleed Malik kutoka Benki ya Dunia, wa nne kulia ni Bw. Denis Biseko-Benki ya Dunia-Tanzania, wa tatu kushoto ni Mtendaji wa Mahakama ya Rufani, Bw. Sollanus Nyimbi, wa tatu kulia ni Mhe. Zahra Maruma, Mkuu wa Kitengo cha Maboresho, Mahakama ya Tanzania (JDU) pamoja na Wajumbe wengine kutoka Mahakama walioshiriki katika mazungumzo hayo.
 Wajumbe kutoka Benki ya Dunia wakiwa ndani ya Mahakama inayotembea ‘mobile court’ iliyopo mkoani Mwanza, lengo ni kujionea hali ya ufanyaji kazi wa Mahakama hiyo.
 Picha ya pamoja kati ya Ujumbe wa Benki ya Dunia pamoja na baadhi ya Wasajili na Watendaji wa Mahakama mbele ya jengo la Mahakama Kuu Musoma-Mara. Jengo hili pia lilikaguliwa na Ujumbe huo.
Jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu lililokaguliwa na Ujumbe kutoka Benki ya Dunia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad