TUZO ZA "TANZANIA ELIMU AWARDS" KUTOLEWA AGOSTI 31 MWAKA HUU - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 27 August 2019

TUZO ZA "TANZANIA ELIMU AWARDS" KUTOLEWA AGOSTI 31 MWAKA HUU

* Wanafunzi, walimu na wadau mbalimbali wanaoshiriki kuiinua sekta ya elimu kupata tuzo hizo

KWA mara ya kwanza Kampuni ya Elimu Solutions Tanzania imeandaa tuzo za Tanzania Elimu Awards zitakazotolewa  Agosti 31 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam huku mgeni rasmi akitegemewa kuwa Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Seleiman Jaffo (Mbunge.)

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Elimu Solution nchini Neithan Swedi amesema kuwa jukumu la kusaidia sekta ya elimu ni la kwetu zote, na serikali imeonesha mfano kwa kushiriki vyema katika sekta ya elimu na mwaka huu shule za serikali zimeingia katika shule kumi bora zilizofanya vizuri zaidi katika mitihani ya kidato cha sita.

Amesema kuwa wameanzisha utoaji tuzo za Tanzania Elimu Awards kwa walimu, wanafunzi na wadau wa sekta hiyo Afrika Mashariki na hiyo ni katika kuendeleza na kusimamia sekta hiyo muhimu katika ujenzi wa taifa na kueleza kuwa ni muhimu kuendeleza sekta hiyo ili iendelee kuwa kiwanda cha kuzalisha vijana wa kitanzania ambao ndio taifa la kesho.

Kwa upande wake msimamizi wa miradi kutoka Elimu Solutions Tanzania Peter Godian amesema kuwa katika kuenzi na kuheshimu jitihada za wanafunzi, walimu, shule, serikali na taasisi mbalimbali kampuni hiyo kwa mara kwanza imeandaa tuzo hizo ili kuleta motisha ili kuipeleka sekta hiyo mbele zaidi.

Amesema kuwa tuzo hizo TEA  zinajumuisha tuzo 32 kutoka vipengele vikuu 11 zikiwemo tuzo kwa wanafunzi Bora wakike na kiume kwa shule za msingi na sekondari pamoja na vipengele mbalimbali vikiwemo walimu bora, shule bora, na tuzo ya heshima.

Amesema kuwa washindi watapatikana kupitia takwimu zitakazopatikama kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu na wanaamini itachangia katika kuchangia utamaduni wa kutunza na kutambua mchango wa wasomi, wabunifu na wadau wa sekta ya elimu na kuzidi kuwapa faraja na moyo wa kuendelea kufanya kazi na kukuza sekta adhimu ya elimu.
  Mkurugenzi Mtendaji wa  Elimu Solutions Tanzania Neithan Swedi akizungumzia kuhusu utoaji wa Tuzo zijulikanazo kama Tanzania Elimu Awards zitakazotolewa na Kampuni hiyo zitakazofanyika Agosti 31, 2019 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msimamizi wa Miradi kutoka Elimu Solutions Tanzania Peter Godian na Kulia ni Afisa Masoko wa  Elimu Solutions Tanzania Catherine Ndosi.
 Msimamizi wa Miradi kutoka Elimu Solutions Tanzania Peter Godian akisoma tuzo zitakazotolewa  na kampuni ya Elimu Solutions Tanzania kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo zijulikanazo kama Tanzania Elimu Awards zitakazofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Masoko wa  Elimu Solutions Tanzania Catherine Ndosi na kushoto ni  Mkurugenzi Mtendaji wa  Elimu Solutions Tanzania Neithan Swedi.
 Afisa Masoko wa  Elimu Solutions Tanzania Catherine Ndosi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kapuni hiyo ilivyojipanga kutekeleza utoaji wa tuzo hizo wakati wa kutangaza utoaji wa tuzi zijulikanazo kama Tanzania Elimu Awards

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad