BENKI ya Standard Chartered jana imezindua huduma mpya ya fedha kwa wateja wake wakubwa, ambao wataweka fedha hizo katika akaunti zao kwa kutumia mashine maalumu (Cash Deposit Machines services-CDMs) zitakazowekwa kwenye eneo la biashara.
Huduma hiyo ni juhudi za benki hiyo kutekeleza matakwa ya wateja wake ya kuwa karibu nao na kurahisisha uwekaji wa fedha na usalama wake.
Huduma hiyo ambayo inawezesha mteja kuwa na mtambo wa kuwekea fedha katika eneo lake la kazi (Cash Deposit Machines services-CDMs) imelenga kwa wafanyabiashara wakubwa kama wenye vituo vya mafuta, maduka makuu, na wauzaji wa vinywaji baridi.
Imeelezwa kuwa CDMs hizo zitafungwa katika maeneo ya biashara hizo na kutoa huduma za kuhifadhi fedha muda wowote ule.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi huo wa huduma za CDMs, Mkuu wa Kitengo cha huduma za kibenki kwa Mashirika, Biashara na taasisi za kifedha, Bw. James Meitaron, alisema: “ Benki ya Standard Chartered inazindua Cash Deposit Machines ili kuwezesha wateja wetu wakubwa kuwa na muda zaidi wa kushughulika na kazi na kuacha shaka ya upelekaji wa fedha nyingi kila mara. kwa kuwa na CDMs wateja wetu sasa wanaweza kuhifadhi fedha katika akaunti zao muda wowote katika mtambo huo. fedha zinazowekwa zitaonesha katika kumbukumbu za kibenki.”
Aidha alisema kwamba CDMs imeunganishwa na mifumio mingine ya kibenki ya kidigitali ikiwamo Bank’s Corporate Banking Digital platform, S2B, hivyo kumwezesha mteja kuona kinachoendelea katika akaunti yake.
Akizungumzia usalama wa mitambo hiyo, Meitaron alisema kwamba benki inawajibika mara tu fedha hizo zinapowekwa katika mitambo ya CDMs. Pia benki ndiyo itakayosafirisha fedha hizo kutoka katika eneo la mteja hadi benki.
Mitambo hiyo itawekwa katika maeneo ya mteja yaliyo salama huku hatua zote za kiusalama zikiwa zimetekelezwa.
Pia mitambo hiyo ina uwezo wa kutambua fedha za bandia na kwamba zitakuwa zinaangaliwa na watu ambao watachaguliwa na wateja wenyewe.
“baadhi ya wateja wetu wana huduma hizi na wameomba mitambo zaidi kutokana na haja kutunza muda na usalama wa fedha. Nashauri wateja wengi kujaribu huduma hii watafurahi,” alisema Meitaron
Uzinduzi wa CDMs unafanyika ikiwa ni sehemu ya harakati za benki za kufikia wateja wake pale walipo kwa kutumia njia mbalimbali. Hivi karibuni benki hiyo ilizindua Full Digital Bank on Mobile kwa ajili ya wateja wadogo binafsi na hii ya CDMs ni kwa ajili ya wateja wakubwa.
Mkuu
wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi.
Juanita Mramba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kabla
ya kumkaribisha Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki kwa Makampuni
makubwa, ya kati na taasisi za kifedha wa Benki ya Standard Chartered
nchini, Bw. James Meitaron wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma
mpya ya fedha kwa wateja wake wakubwa ya kuweka fedha katika akaunti zao
kwa kutumia mashine maalumu (Cash Deposit Machines services-CDMs)
zitakazowekwa kwenye eneo la kazi uliofanyika Hoteli ya Hyatt-The
Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Bidhaa za makampuni
makubwa na ya kati wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Busara
Raymond.
Mkuu
wa Kitengo cha Huduma za Kibenki kwa Makampuni makubwa, ya kati na
taasisi za kifedha wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. James
Meitaron akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu
huduma mpya ya fedha kwa wateja wake wakubwa ya kuweka fedha katika
akaunti zao kwa kutumia mashine maalumu (Cash Deposit Machines
services-CDMs) zitakazowekwa kwenye eneo la kazi wakati wa hafla fupi
ya uzinduzi iliyofanyika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Meneja Bidhaa wa makampuni makubwa na ya kati wa
Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Busara Raymond na kulia ni Mkuu
wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi.
Juanita Mramba.
Meneja
Bidhaa wa makampuni makubwa na ya kati wa Benki ya Standard Chartered
nchini, Bw. Busara Raymond akizungumza jambo na waandishi wa habari
(hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma mpya ya
fedha kwa wateja wake wakubwa ya kuweka fedha katika akaunti zao kwa
kutumia mashine maalumu (Cash Deposit Machines services-CDMs)
zitakazowekwa kwenye eneo la kazi uliofanyika Hoteli ya Hyatt-The
Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma
za Kibenki kwa Makampuni makubwa, ya kati na taasisi za kifedha wa
Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. James Meitaron na kulia ni Mkuu
wa Mahusiano na Masoko wa benki hiyo, Bi. Juanita Mramba.
Baadhi
ya mashine maalumu za kuweka fedha (Cash Deposit Machines
services-CDMs) zitakazowekwa kwenye eneo la kazi kabla ya kuzinduliwa
rasmi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika katika Hoteli ya
Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
Meneja
Bidhaa wa makampuni makubwa na ya kati wa Benki ya Standard Chartered
nchini, Bw. Busara Raymond (kulia) akitoa maelezo kwa waandishi wa
habari (hawapo pichani) jinsi mashine maalumu ya kuweka fedha (Cash
Deposit Machines services-CDMs) kwenye eneo la kazi inavyofanyakazi
wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma mpya ya fedha kwa wateja wake
wakubwa uliofanyika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki kwa Makampuni
makubwa, ya kati na taasisi za kifedha wa Benki ya Standard Chartered
nchini, Bw. James Meitaron.
Mkuu
wa Kitengo cha Huduma za Kibenki kwa Makampuni makubwa, ya kati na
taasisi za kifedha wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. James
Meitaron akikata utepe ishara ya kuzindua rasmi mashine maalumu ya
kuweka fedha (Cash Deposit Machines services-CDMs) kwenye eneo la kazi
wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma mpya ya fedha kwa wateja wake
wakubwa uliofanyika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es
Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Meneja Bidhaa wa makampuni makubwa
na ya kati wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Busara Raymond
pamoja na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa benki hiyo, Bi. Juanita Mramba.
Mkuu
wa Kitengo cha Huduma za Kibenki kwa Makampuni makubwa, ya kati na
taasisi za kifedha wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. James
Meitaron (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani) mara baada ya kuzindua mashine maalumu za kuweka fedha (Cash
Deposit Machines services-CDMs) kwenye eneo la kazi wakati wa hafla fupi
ya uzinduzi wa huduma mpya ya fedha kwa wateja wake wakubwa uliofanyika
Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu
wa Mahusiano na Masoko wa benki hiyo, Bi. Juanita Mramba na kulia ni
Meneja Bidhaa wa makampuni makubwa na ya kati wa Benki ya Standard
Chartered nchini, Bw. Busara Raymond.
Mpiga
picha wa gazeti la Mwananchi, Said Nanjundo akiuliza swali kwa uongozi
wa Benki ya Standard Chartered wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa
huduma mpya ya fedha kwa wateja wake wakubwa ya kuweka fedha katika
akaunti zao kwa kutumia mashine maalumu (Cash Deposit Machines
services-CDMs) zitakazowekwa kwenye eneo la kazi uliofanyika Hoteli ya
Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Kitengo cha Huduma za Kibenki kwa Makampuni makubwa, ya kati na
taasisi za kifedha wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. James
Meitaron katika picha na moja ya mashine maalumu ya kuweka fedha (Cash
Deposit Machines services-CDMs) kwenye eneo la kazi wakati wa hafla fupi
ya uzinduzi wa huduma mpya ya fedha kwa wateja wake wakubwa uliofanyika
Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment