Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
amelitaka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuhulikia Wanawake Duniani
(UN WOMAN) kuandaa Tathmini ya kinchi kuhusiana na Kongamano la
Beijing.
Amesema
ni Vyema kuwepo na uwezekano wa kuweza kuandaa Tathmini ya uhakika
itakayoweza kuonesha hali halisi ya Idadi ya Wanawake waliopo katika
Nafasi mbalimbali za Kiuongozi hususan kwenye Baadhi ya Mashirika na
Taasisi Binafsi.
Makamu
wa Rais ameyasema hayo leo Agost 14, 2019 Ofisini kwake Ikulu Jijini
Dar Es Salaam wakati alipokutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkazi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuhulikia Wanawake Duniani (UN WOMAN)
Bibi Hodan Addou.
Aidha
Makamu wa Rais amelishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshuhulikia Wanawake Duniani (UN WOMAN) kwa kuendelea kuweza kutoa
fursa katika nyanja mbalimbali za Kijamii na kimaendeleo kwa Wanawake
Duniani na kulitaka Shirika hilo kuendelea kuzidi kutoa fursa hizo kwa
Wanawake Hususan kwenye sekta za Kilimo.
Nae
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuhulikia
Wanawake Duniani Bibi Hodan Addou aliyeambatana na Bw. Denis Maro Biseko
Mwakilishi wa Benki ya Dunia hapa Nchini, amemshukuru Mhe. Makamu wa
Rais kwa kuweza kuimarisha Ulizi wa Masoko kwa kuzuwia Utumikishaji wa
Wanawake na watoto Masokoni. Ambapo pia amesema Shirika hilo kwa
kushirikiana na Benki ya Dunia wameandaa Warsha itakayozungumzia kuhusu
Wanawake kuweza kutambua hali zao kwenye suala zima la Biashara.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisalimina na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshuhulikia Wanawake Duniani(UN WOMAN) Bibi. Hodan Addou wakati
Bibi Addou alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar Es
Salaam leo Agost 14,2019 kwa ajili ya kumshukuru Makamu wa Rais kwa
kuweza kuimarisha Ulizi wa Masoko kwa kuzuwia Utumikishaji wa Wanawake
na watoto Masokoni ambapo pia amesema Shirika hilo kwa kushirikiana na
Benki ya Dunia wameandaa Warsha itakayozungumzia kuhusu Wanawake kuweza
kutambua hali zao kwenye suala zima la Biashara.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshuhulikia Wanawake Duniani (UN WOMAN) Bibi. Hodan Addou wakati
Bibi Addou alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar Es
Salaam leo Agost 14,2019 kwa ajili ya kumshukuru Makamu wa Rais kwa
kuweza kuimarisha Ulizi wa Masoko kwa kuzuwia Utumikishaji wa Wanawake
na watoto Masokoni ambapo pia amesema Shirika hilo kwa kushirikiana na
Benki ya Dunia wameandaa Warsha itakayozungumzia kuhusu Wanawake kuweza
kutambua hali zao kwenye suala zima la Biashara.
No comments:
Post a Comment