HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 3, 2019

WIZARA YA VIWANDA YAJIPANGA KUKUZA MASOKO NDANI NA NJE YA NCHI

*Yatakiwa kuwa karibu na balozi zilizopo nchini ili kuweza kupata masoko ya bidhaa za ndani

*TANTRADE wapongezwa kwa kuyatendea haki maonesho hayo kila mwaka

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MAONESHO ya 43 ya biashara maarufu kama sabasaba yenye  kauli mbiu ya usindikaji wa mazao ya kilimo kwa maendeleo ya viwanda yamezinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam huku masuala ya utafutaji wa masoko pamoja na kuelimimisha wafanyabiashara kuhusiana na kliniki ya biashara yakitiliwa mkazo.

Akizungumza katika ufunguzi huo makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa maonesho hayo ni kwa kutoa kipaumbele kwa bidhaa zinazozalishwa nchini Kama Rais anavyosisitiza.

Suluhu amesema kuwa maonesho ya sabasaba ni makubwa katika ukanda wa Afrika na katika maonesho hayo zaidi ya nchi 35 zimeshiriki katika hali inayoashiria ubora na utulivu unaovutia uwekezaji katika nchi yetu.

Amesema kuwa serikali itaviwezesha viwanda vidogo na Kati katika masoko pamoja na kuendelea kushiriki katika maonesho hayo ili waweze kutangaza bidhaa zao zaidi.

Pia amesema kuwa kukua kwa uchumi kwa asilimia 7 kunachagizwa na maendeleo ya viwanda na kasi zaidi pamoja na wasimamizi wa sekta hiyo utapelekea wananchi kufanana na kasi ya ukuaji wa uchumi.

Aidha amezitaka mamlaka za TFDA, TBS, mamlaka za uvuvi na kilimo kufanya kazi kwa uadilifu na utii na wao kama Serikali watasimamia na kuhakikisha hakuna urasimu katika hilo, na amewahimiza tantrade ambao ndio wasimamizi na waandaaji wa maonesho hayo kutafuta masoko na kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na ubora na kuhamasisha matumizi ya bidhaa zinazozalishwa nchini.

Kuhusiana na ujenzi wa viwanda Suluhu amesema kuwa azma ya serikali katika ujenzi wa viwanda bado ipo palepale na hiyo ni pamoja na utafutaji wa masoko ya ndani na nje.

Kwa upande wake Katibu mkuu wa chama Cha mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally amewapongeza bodi, baraza na wafanyakazi wa tantrade kwa kuyatendea haki maonesho hayo mwaka hadi mwaka.

Amesema kuwa maonesho ya namna hayo ni kisiwa Cha kuboresha nyaraka za kisera zinazosaidia katika maendeleo.

Pia Waziri wa viwanda na biashara Innocent Bashungwa amesema kuwa gurudumu la maendeleo linaenda vyema na hiyo ni kutokana na uongozi Bora wa serikali ya awamu ya tano na kusema kuwa wizara za biashara na viwanda pamoja na uvuvi na kilimo  zinategemewa na watanzania wengi hivyo zitazidi kusimamiwa ili kuongea kipato zaidi.

Bashungwa amehaidi ushirikiano baina yao na wawekezaji na ndani na nje ya nchi na kuwahimiza watanzania kushiriki katika ujenzi wa taifa kwa kujihusisha na viwanda hasa vidogo na vya Kati.

Aidha amezitaka halmashauri zote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji na wao Kama wizara watahakikisha uwepo wamaeneo ya usindikaji.

Ufunguzi huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri, wakuu wa Wilaya, wabunge pamoja na wajumbe wa baraza la wawakilishi.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza wakati wa uzindua rasmi wa maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara katika Viwanja vya Sabasaba Barabara ya kilwarod jijini Dar es salaam leo Julai 02, 2019. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua rasmi kwa kubonyeza kitufe maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara katika Viwanja vya Sabasaba Barabara ya kilwarod jijini Dar es salaam Julai 02, 2019. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa zawadi kwa washindi wakati wa uzinduzi rasmi na kutembelea maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara katika Viwanja vya Sabasaba Barabara ya kilwarod jijini Dar es salaam Julai 02, 2019. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,  akitembelea mabanda mablimbali mara baada ya kuzindua rasmi maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara katika Viwanja vya Sabasaba Barabara ya kilwarod jijini Dar es salaam Julai 02, 2019. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad