HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 3, 2019

WAZIRI WA UJENZI, MHANDISI KAMWELE AFANYA MAZUNGUMZO NA WACHIMBAJI WA MADINI WAKUBWA ILI KUTATUA CHANGAMOTO ZAO

 Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele akizungumza na wachimbaji wa madini wakubwa Duniani ili waweze kuitumia Bandari ya Dar es Salaam inayoendelea kupanuliwa pamoja na wachimbaji hao kueleza kueleza changamoto wanazozipata ili waweze kutumia Bandari hiyo na kurahisiha mizigo kupita kwa haraka na bila usumbufu wowote ili kufikia malengo waliyojiwekea katika bandari hiyo.

 Baadhi ya wachimbaji wakubwa wa madini wakiwasilisha changamoto kwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele wanazozipata pale wanapotumia bandari ya Dar es Salaam wakati wa kikao kilichoandaliwa na Waziri huyo ili kutatua changamoto hizo ikiwemo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

Naibu Waziri Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya akifuatilia kikao kilichojumuisha wachimbaji wa Madini wakubwa pamoja Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele  kilichokuwa na lengo la kusikiliza changamoto wanazozipata wachimbaji hao ili waweze kutumia bandari ya Dar es Salaam kwa asilimia 100.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akitolea ufafanuzi baadhi ya hoja za wachimbaji wa madini zilizowasilishwa kwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele  wakati wa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa TPA jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), wizara na wachimbaji wa Madini wakiwa kwenye kikao kilichoitishwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele ili kusikiliza changamoto wanazozipata wachimbaji hao wanapotumia Bandari ya Dar es Salaam.
 Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele akizungumza na waandishi wa khusu lengo la Serikali kuitisha kikao na Wachimbaji wa Madini wakubwa Duniani ili kuweza kusikiliza changamoto wanazozipata wanapotumia Bandari ya Dar es Salaam pamoja na kuzitafutia ufumbuzi ili waweze kutumia Bandari hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mamlaka hiyo ilivyojipanga kuhudumia wateja wao kwa ufanisi ili kufikia malengo waliyojiwekea kuelekea Uchumi wa Viwanda.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad