HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 17, 2019

WAZIRI MKUU MAJALIWA APONGEZA UTENDAJI WA PSPTB

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepongeza utendaji wa Bodi ya PSPTB na kueleza umuhimu wa kuundwa kwa Bodi hiyo ni pamoja na kusaidia wadau wapate   bidhaa kwa wakati na kulingana na thamani ya pesa zao.

Aliongea hayo wakati alipotembelea banda la PSPTB na kuelezwa majukumu ya Bodi hiyo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Godfred Mbanyi na hayimaye kukabidhiwa jarida lenye kuonesha kazi mbalimbali zilizofanya na PSPTB na muundo mzima wa Bodi ya wakurugenzi na menejimenti ya PSPTB. 

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma moja ya jarida kwenye banda la bodi ya ununuzi na ugavi(PSPTB) kuhusu  jinsi bodi hiyo inavyofanya kazi wakati wa ufunguzi wa wa Maonesho ya Vyuo vikuu yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa bodi ya ununuzi na ugavi(PSPTB) Godfred Mbanyi  
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa bodi ya ununuzi na ugavi(PSPTB) Godfred Mbanyi(katikati) kuhusu mfumo wa usajili na jinsi bodi hiyo inavyofanya kazi wakati wa ufunguzi wa wa Maonesho ya Vyuo vikuu yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad