NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
WATU wawili wamefariki dunia mkoani Pwani ,kutokana na matukio tofauti
ya mauaji yaliyotokea wilaya ya kipolisi Chalinze, ikiwa ni pamoja na
Damian Kimiti (70) ambae ameuawa kwa kupigwa shoka.
Kufuatia mauaji hayo watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapo.
Akielezea kuhusiana na matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani hapo,
kamanda wa polisi wa mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa alisema Kimiti
aliuawa huko Malivundo, Talawanda, Chalinze, ambapo mtiliwa shaka Said
Ngosha amekubali kuuwa na tayari amekamatwa .
Alisema, baada ya mauaji muaji alipora simu tatu aina ya tecno ,solar
panel moja,shuka na baiskeli. "Pia alikubali kuonyesha simu tecno mbili ,solar panel moja na shoka
moja"alifafanua Wankyo.
Katika tukio jingine ,Wankyo alieleza Ngurai Waziri (33) mfugaji huko
Msolwa kijiji cha Lukenge aliuawa kwa kukatwa na visu.

Kamanda huyo alibainisha, mtiliwa shaka David Mwanje (28) , Thomas Gau
(25) na Magoma Ramadhani Mbwiga (32) wamekamatwa na katika mahojiano
ya awali watuhumiwa hao wamedai marehemu alikuwa mwizi wa mifugo na
alikuwa kero katika wizi wa mifugo.
Wakati huo huo Wankyo alisema, juni 30 eneo la Sweat Corner Vigwaza
katika barabara kuu ya Morogoro -Dar es salaam ,gari lenye namba za
usajili T.182 DGH/T .182 DGM aina ya scania ,lililokuwa likitokea
Iringa kuelekea Dar es salaam likiendeshwa na dereva Samwel Emanuel
mkazi wa Makambako Iringa.
"Gari hilo liligongana uso kwa uso na gari lenye namba za usajili
T.420 CGK/T.909 BZU scania lililokuwa likitokea Dar es salaam kuelekea
Chalinze likiendeshwa na Iddi Rashid mkazi wa Tegeta ikiwa imebeba
malighafi zitumikazo kutengeneza juice na kusababisha moto mkubwa na
magari yote yaliteketea."aliongeza Wankyo.
Wankyo alitaja chanzo cha ajali ni gari lenye namba T.420 CGK aina ya
scania kuhama upande wake na kuhamia upande wa kulia mwa barabara.
No comments:
Post a Comment