HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 15, 2019

WATANZANIA WATAKIWA KUCHAGUA VIONGOZI WA MITAA WANAOWEZA KUPAMBANA NA MIMBA ZA UTOTONI

WAKATI taifa linajiandaa kuelekea katika uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa, wito umetolewa kwa wananchi kuhakikisha wanatumia haki yao ya msingi kwa kupiga kura na kuchagua viongozi wenye hofu ya Mungu na wanaojali haki za watoto wa kike.

Hayo yameelezwa na Mratibu wa Shirika la utetezi wa haki za mtoto wa kike la New Hope nchini Bi. Elizabeth Ngaiza ambapo amesema kuwa katika kampeni ya "Niache Nisome Kwanza" anayoiendesha amebaini uwepo wa baadhi ya viongozi wa ngazi za mitaa wasiokuwa na weledi, wasiowajibika na hawawezi kusimama katika nafasi a na kutetea haki za mtoto wa kike.

Aidha bi Elizabeth Ngaiza amesema, lengo la Kampeni ya "Niache Nisome Kwanza" ni kupambana na mimba za utotoni kwa mtoto wa kike na kuhakikisha anawekewa mazingira wezeshi ya kusoma pasipo changamoto wala vikwazo vyovyote.

Hata hivyo  amewaomba wadau na wananchi kuendelea kumuunga mkono katika Kampeni ya kumlinda mtoto wa kike ili apate elimu bora kwakuwa anaamini ukimwezesha mwanamke kupata elimu itasaidia kuinua kipato cha familia na taifa kwa ujumla.
 Mratibu  wa shirika la kutetea haki za mtoto wa kike la New Hope, Elizabeth Ngaiza akizungumza wakati wa warsha hiyo, ambayo amewataka wananchi kuchagua viongozi wenye weledi na wenye hofu ya Mungu, leo jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad