HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 7 July 2019

WANACHAMA PSSSF WAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUFUATILIA TAARIFA ZA MICHANGO YAO

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WASTAAFU watarajiwa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wameaswa kujenga utamaduni wa kufuatilia taarifa za michango yao mara kwa mara ili kujipanga vema wakati wa kustaafu unapowadia, Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma (CMPR), wa Mfuko huo, Bi. Eunice Chiume amesema.

Bi Chiume ameyasema hayo Julai 7, 2019 wakati akiungana na watumishi wenzake wa Mfuko kuhudumia wanachama wanaofika kupata huduma kwenye banda la PSSSF kwenye Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ambapo watu wengi hususan wale wanaotarajia kustaafu wamekuwa wakijitokeza ili kujua taarifa za michango yao.

Wanachama na wananchi wanahamasishwa kutembela banda hilo ili kupata huduma na taarifa mbalimbali kuhusu shughuli za Mfuko ambao umeundwa baada ya kuunganishwa kwa Mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ya GEPF, PSPF, LAPF na PPF. 

Huduma zitolewazo na PSSSF kwenye banda hilo namba 13 ambalo pia linatumiwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), ni pamoja na taarifa za Uhakiki wa wastaafu, taarifa za Pensheni ya Uzee, taarifa za Mafao ya kukosa Ajira, taarifa za Mafao ya Uzazi, taarifa za Dhamana ya Mikopo ya Nyumba na na taarifa za Uwekezaji. Maonesho hayo yaliyoanza Juni 28, 2019 yanatarajiwa kufikia kilele Julai 13, 2019 ambapo Kauli mbiu ya mwaka huu ni "Usindikaji wa Mazao ya Kilimo kwa Maendeleo Endelevu ya Viwanda."
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), David Misiime ambaye ni mwanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), akipitia taarifa ya michango yake huku akipata usaidizi kutoka Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko huo, Bi. Eunice Chiume Julai 7, 2019 wakati alipotembelea banda la PSSSF kwenye viwanja vya Julius Nyerere (Sabasaba) wakati wa maonesho ya 43 ya biashara ya Kimata ya Dar es Salaam yanayoendelea kwenye viwanja hivyo.
Afisa Mwandamizi wa Malipo, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma,(PSSSF), Bi.Nyangi Masalu (kushoto), akimuhudumia mwananchi aliyetembelea banda la PSSSF Julai 7, 2019.
Afisa Uhusiano Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Fatma Elhady, na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi, wakiwasilkiliza wananchi waliotembelea banda la Mfuko huo Julai 7, 2019.
Hakika mama ni mama: Afisa Mwandamizi wa Malipo, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bi.Nyangi Masalu (kulia), akimbembeleza kichanga huyu huku mama yake akiwa karibu wakayi Nyangi alipomalzia kumuhudumia mume wa mama huyo aliyetembeela banda la PSSSF.
Afisa Mwandamizi wa Malipo, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma,(PSSSF), Bi.Nyangi Masalu (kulia), akimsikilzia Mwanachama aliyetembelea banda la Mfuko huo.
Mwnaachama wa PSSSF akimsikliza Afisa wa PSSSF wakati alipofika kwenye banda la Mfuko huo ili kuhudumiwa.
Afisa Uhusiano Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Fatma Elhady, akimsikiliza mwanachama huyu aliyetembelea banda la PSSSF Julai 7, 2019.
Afisa Michango PSSSF Bi. Getrude Athanas (kulia), akimsikiliza mwanachama huyu aliyefika na familia yake kupata taarifa za michango yake.
Afisa Mafao PSSSF, Bw. Salvatory Matemu akimsikiliza mwanachama huyu aliyefika kuhudumiwa.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad