HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 11, 2019

TCRA kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wamekamata watu 14 wanaondesha usajili laini simu

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeendesha operesheni wahudumu 14 wanaosajili watu kwa kutumia alama za vidole bila kuwa na vitambulisho vya watoa huduma vya Kampuni za simu.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa waliokamatwa wanatakiwa mashitaka kutokana na kutumia mashine za kusajili alama za vidole bila kuwa kitambulisho cha mtoa huduma Kampuni ya simu husika.
Operesheni hiyo leo imeendeshwa katika Kanda zote za TCRA kwa watu wanaoendesha usajili wa alama za vidole bila kuwa vitambulisho vya watoa huduma.

Amesema ni kosa la kisheria kuendesha usajili wa laini za simu bila kuwa na kitambulisho na kuongeza kuwa baadhi yao wanafanya udanganyifu kwa wananchi kwa kuwatoza fedha.
Amesema mawakala waliowapa mashine  hizo wamefanya kosa la kisheria kwa utoaji wa mashine hizo kiholela.

Mhandisi Odiero amesema walishatoa namna ya usajili hivyo lakini baadhi wamekiuka utaratibu huo hivyo sheria lazima ishike mkondo wake.
Aidha ameongeza kuwa operesheni hiyo ni endelevu na kuwataka watoa huduma za usajili wakiwa na mashine kuacha ni mpaka pale watapokuwa na vitambulisho vya watoa huduma wa Kampuni za simu.
 Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero akizungumza kuhusiana na operesheni ya kuwakamata wanaoendesha huduma za usajili laini ya bila na vitambulisho kutoka Kwa watoa huduma wa Kampuni za simu ,jijini Dar es Salaam.
 Afisa wa TCRA pamoja na Afisa wa Polisi wakichukua taarifa za mtoa huduma za usajili wa laini za simu kwa za vidole ambapo amekamatwa na Polisi kwa kuendesha huduma hiyo bila kuwa na kitambulisho cha Kampuni ya simu ya kumtambulisha kufanya huduma hiyo katika maeneo ya kariokoo jijini Dar es Salaam.
Afisa wa TCRA Noah Lalataika akichukua maelezo ya mtoa huduma za usajili wa laini ambapo anaendesha huduma hiyo bila ya kuwa na kitambulisho cha kumtambulisha kufanya huduma ya usajili wa laini kutoka Kampuni za simu katika eneo la Kariokoo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad