HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 1, 2019

TAKUKURU Dodoma yabaini vitendo vya rushwa Chemba

Na Charles James, Michuzi TV
TAASISI ya kizuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Dodoma imeingilia kati ujenzi wa mradi wa maji wa Kijiji cha Kelema Kuu wilayani Chemba baada ya kubaini thamani ya fedha iliyotumika kutoendana na kazi halisi iliyofanyika.

Aidha mradi huo wenye thamani ya shilingi 222,978,680 ulipaswa kukamilika tangu mwaka 2015.

Hatua hiyo imefanyika ikiwa ni utekelezaji wa moja ya majukumu yake chini ya kifungu cha 7 cha Sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa ya mwaka 2007.

Hayo yamebainishwa Julai mosi mwaka huu  jijini Dodoma na Mkuu wa TAKUKURU Dodoma Sosthenes Kibwengo wakati akitoa taarifa kwa umma juu ya vitendo vya rushwa katika robo ya mwezi April hadi Juni.

Aidha Kibwengo amesema ,katika uchunguzi huo ilibainika kuwa thamani ya fedha haikupatikana kutokana na uwepo wa malipo zidifu ya kazi halisi zilizofanyika na kutandikwa kwa aina ya mabomba kinyume na mkataba hivyo kusababisha mradi huo kutokutoa maji.

"Baada ya TAKUKURU kuingilia kati ,mkandarasi wa mradi huo JUIN COMPANY LIMITED ameridhia kurekebisha mapungufu yaliyobainika na leo hulali mosi anaanza kazi ya kubadili mabomba na kuweka yanayostahili,"alisema.

Pamoja na hayo amesema Mkandarasi huyu atarejesha malipo zidifu yaliyolipwa bila kustahili .

"Jumla ya shilingi 67,542,600/= zimeokolewa na tunatarajia wananchi watapata huduma ya maji ,"alisema Kibwengo.

Katika hatua nyingine taasisi hiyo imemkamata Be.Gaston Meltus Francis ambaye ni mkurugenzi wa Global Space East Afrika Limited iliyopewa kazi ya ujenzi wa kituo cha afya Mima wilayani Mpwapwa ambapo kampuni yake ililipwa kiasi cha shilingi 86,405,205 isivyo halali kwa kazi ambazo hazikufanyika katika mradi huo.

Kwa mujibu wa mkuu wa TAKUKURU Dodoma ,uchunguzi huo umeokoa na kurejesha Serikalini jumla ya shilingi 11,877,353 /=zilizolipwa kinyume na taratibu Kama mshahara kwenye akaunti ya benki ya mwalimu aliyefariki.

Aidha kufuatia matukio hayo , TAKUKURU mkoa wa Dodoma inawataka wananchi wote kuendelea kutoa ushirikiano na kuwaomba wasiwe watazaji bali washiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya rushwa.

"Tunawataka wanajamii kuwa waangalifu na kamwe wasikubali kurubuniwa na matapeli wanaojifanya maofisa wa TAKUKURU wanaowapigia simu na kuwatisha bali watoe taarifa kupitia namba 113 au kufika katika Ofisi zetu,"alisema Kibwengo.
Kamanda wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo, akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad