Naibu
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana,
Antony Mavunde (wa pili kushoto), akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi
milioni nne kwa mshindi wa kwanza wa shindano la michoro ya usalama
barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi mwaka 2019, Alphonce Philipo
wa shule ya msingi Jenerali Musuguri, katika hafla iliyofanyika jijini
Dodoma jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania,
waandaaji wa shindano, Dominic Dhanah

Naibu
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana,
Antony Mavunde,akizungumza wakati wa kutoa zawadi kwa wanafunzi wa shule
za msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa
mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika
katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .

Mkurugenzi
Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, waandaaji wa shindano, Dominic
Dhanah,akisoma taarifa katika utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wa shule za
msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka
2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika
shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .

Mkurugenzi
Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, waandaaji wa shindano, Dominic
Dhanah,akifurahia jambo na wanafunzi (hawapo pichani) wakati akisoma
taarifa inayohusu utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi
walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019
yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika
shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .

Mratibu
wa mafunzo ya Elimu ya usalama barabarani kutoka Amend Bi.Neema
Swai,akiongea wakati wa kutoa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi
walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019
yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika
shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .

Mwalimu
wa shule ya Msingi ya General Musuguri,Beatrice Chidumizi,akitoa
pongeza kwa Puma Energy wakati wa kutoa zawadi kwa wanafunzi wa shule za
msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka
2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika
shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .

Afisa
Elimu Msingi jiji la Dodoma,Joseph Mabeyo,akitoa shukrani kwa Kampuni
ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania wakati wa kutoa zawadi kwa wanafunzi
wa shule za msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani
kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo
imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .

Naibu
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana,
Antony Mavunde (wa pili kulia), akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa
Puma Energy Tanzania, waandaaji wa shindano, Dominic Dhanah, wakati wa
kutoa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la
Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma
Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni
jijini Dodoma .

Mwalimu
wa shule ya msingi Kaloleni Bi.Edina Kagulumbega,akizungumza wakati wa
kutoa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la
Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma
Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni
jijini Dodoma .



Sehemu
ya Wanafunzi kutoka shule za msingi wakifuatilia hafla ya utoaji wa
zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la Michoro
ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy
Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini
Dodoma .

Baadhi
ya walimu wakifuatilia utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wa shule za
msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka
2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika
shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .

Wanafunzi
wakiimba wimbo maalumu wa unaoelezea umuhimu wa kuzingatia sheria za
usalama barabarani wakati wa utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wa shule za
msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka
2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika
shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .

Mmoja
wa wanafunzi waliopata elimu ya mafunzo ya usalama barabarani akionesha
mfano wa mwanafunzi aliyepata ajali kwa kutozingatia sheria za usalama
barabarani wakati wa utoaji zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi
walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019
yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika
shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .

Wakiangalia
michoro ya usalama barabarani iliyochorwa na wanafunzi kutoka shule
tano za msingi katika jiji la Dodoma kabla ya kumtangaza mshindi wa
shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa
na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi
Kaloleni jijini Dodoma .

Naibu
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana,
Antony Mavunde,akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa shindano la
michoro ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi mwaka
2019, hafla ambayo imefanyika jijini Dodoma.
......................
*Ni katika mkakati wake wa kukomesha ajali nchini, wanafunzi Dodoma wanufaika
*Naibu Waziri Mavunde awapongeza, asema ni kampuni ya mfano...atoa maombi maalum
Na Said Mwishehe,Michuzi TV -Dodoma
KAMPUNI
ya Puma Energy Tanzania imesema itaendelea kutoa elimu ya mafunzo ya
usalama barabarani kwa shule za msingi mbalimbali nchini ikiwa ni
mkakati wake wa kupunguza ajali nchini.
Pamoja
na ahadi hiyo kampuni hiyo imetoa mafunzo ya usalama barabarani kwa
wanafunzi zaidi ya 4500 katika shule tano za msingi katika Jiji la
Dodoma kwa mwaka huu wa 2019 huku ikiahidi kuendelea kutoa elimu hiyo na
kufanya kazi kwa karibu na Serikali ili kuhakikisha elimu hiyo
inawafikia wanafunzi wengi zaidi ambao watakuwa mabalozi kwa wengine.
Akizungumza
leo Julai 25 jijini Dodoma mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Vijana Athony Mavunde, Mkurugenzi Mtendaji
wa Puma Energy Tanzania Dominic Dhanah amesema programu hiyo ya mwezi
mmoja kwa Dodoma ilihusisha mafunzo ya usalama barabarani kwa walimu 15
na wanafunzi 4500, katika shule tano.
Amefafanua
kulikuwa na shindano la uchoraji wa michoro inayo hamsisha usalama
barabarani ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni iliyozinduliwa rasmi
mwaka 2013 ambapo zaidi ya shule 80 zimefikiwa huku wanafunzi 100,000
wakiwa wamepatiwa mafunzo katika mikoa ya Dar-es-salaam, Geita, Ruvuma
na Dodoma.
“Puma
Energy Tanzania imeamua kuja jijini Dodoma kwa sababu ya ukuaji wa
haraka wa jiji hili ambapo shughuli za kijamii na ongezeko la watu na
magari ambayo yanahatarisha usalama wa watoto wanapokwenda shuleni na
kurudi nyumbani,",amesema Dhanah na kuongeza “Hadi sasa tumeweza
kufundisha wanafunzi zaidi ya 4500 wa shule tano za msingi zilizopo jiji
la Dodoma".
Dhahana
amesema mafunzo hayo ya usalama barabarani na uchoraji alama za
barabarani ni kipaumbele kwa lengo la kuwapa uelewa watoto hususani wa
shule za msingi juu ya namna bora ya matumizi ya barabara.Alibainisha
lengo ni kuwafanya watoto kuwa na uelewa wa matumizi ya barabara ili
kuongeza uelewa kuhusu dhima nzima ya usalama barabarani kwa Watanzania.
“Lengo
letu kama kampuni ni kuongeza wigo ili kufikia shule nyingi zaidi nchi
nzima. Puma Energy Tanzania itaendelea kuwekeza katika kampeni ya
usalama barabarani ikishirikiana na serikali kupitia jeshi la Polisi ili
kuokoa maisha ya watanzania,” amebainisha.Akieleza
zaidi amesema unzo hayo yametolewa na Kampuni ya Mafuta ya Puma
Tanzania kupitia Shirika lisilo la kiserikali la Amend ambapo elimu hiyo
pia imetolewa kwa walimu 15 wa shule hizo.
Awa
upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi ,Ajira
na Vijana Anthony Mavunde amesema Puma Energy Tanzania ni kampuni
iliyoamua kutoa elimu ya usalama barabara nchini huku akitoa ombi kwa
kampuni hiyo kufundisha walimu hizo ili wakifundisha masomo ya kawaida
wawe pia wanataka na elimu ya usalama.
Amesema
kwa kufanya hivyo inasaidia kupunguza ama kumaliza kabisa ajali za
barabarani huku akifafanua Serikali itaendelea kuweka alama za usalama
barabarani ili kuondoa changamoto za ajali.Amesema
kuwa kutokea kwa elimu hiyo kwa Jiji la Dodoma kunakwenda kutengeneza
jamii yenye mabalozi wazuri katika kutoa elimu ya usalama barabarani
huku akieleza Dodoma ni ya pili kwa mtandao wa barabara za lamo,hivyo ni
muhimu elimu hiyo kuendelea kutolewa.
"Nimesikia
ombi la walimu na wanafunzi la kuhitaji alama za barabarani, hivyo
Serikali itaendelea kuweka alama hizo.Pia nimezungumza na wenzetu wa
Puma wamekubali kupaka rangi za usalama barabarani na wataanza na shule
tano ambazo zimepatiwa elimu hii ya usalama barabarani,"amesema Mavunde
Wakati
huo huo walimu wakuu katika shule za msingi katika Jiji la Dodoma
wametoa ombi la kuweka alama za barabarani na hasa alama za pundamilia
au matuta ili kuhakikisha wanafunzi wanapovuka wanakuwa salama kwani
barabara nyingi hazina alama hizo.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi General Musuguri Beatrice Chidumizi amesema
changamoto iliyopo kwenye eneo la shule yao ni kukosekana kwa matuta au
alama za barabarani, hivyo wanalazimika kumuweka mtu wa kuvusha
wanafunzi ambaye analipwa fedha.
"Changamoto
kubwa iliyopo katika shule yetu ni barabara yetu kutokuwa na matuta na
alama za pundamilia,hivyo tunaomba tuwekewe alama za barabarani kwa
ajili ya usalama wa wanafunzi wetu.Tunaishukuru Puma kwani imetusaidia
sana kuwajengea uelewa wanafunzi wetu na sasa wanafahamu cha kufanya
wanaoutaka kuvuka barabara.
"Tunaamini
kupitia mafunzo haya tutapunguza ajali kwa watoto wetu na watumiaji
wengine wa barabara zetu,"alisema Mwalimu Chidumizi na kuongeza kuwa
umefika wakati kwa elimu hiyo kuendelea kutokea kwa Jiji la Dodoma hasa
kwa kuzingatia Dodoma inakuwa kwa kasi kutokana na Serikali kuhamia
Dodoma.
No comments:
Post a Comment