HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 18 July 2019

PSPTB yafungua dirisha la usajili

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi bwana Godfred Mbanyi amezindua rasmi mfumo wa usajili kwa njia ya kimtandao.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuzindua mfumo huo bwana Mbanyi amesema kuwa usajili kwa ajili ya mitihani ya mwezi Novemba mwaka 2019 dirisha limefunguliwa na mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 15 mwezi Septemba mwaka 2019. Ameongeza kuwa usajili wa mitihani hiyo hufanyika mara mbili  kwa mwaka yaani mwezi Mei na Novemba.

Mbanyi amesema usajili wa wataalamu wa ununuzi na ugavi hunafanyika mara nne kwa mwaka yaani mwezi Januari, Aprili, Julai na Oktoba.

“Dirisha limeishafunguliwa kwa usajili wa mwezi Oktoba mwaka 2019 na mwisho wa kupokea maombi ni terehe 15 mwezi Septemba mwaka 2019.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB amewataka wadau wote wa Bodi hiyo kutembelea tovuti ya PSPTB ambayo ni www.psptb.go.tz au registration.psptb.go.tz ili waweze kufanikisha usajili wao.

 Pia ametoa rai kwa wadau wa Bodi watakao hitaji maelezo zaidi kuhusu usajili wa mitihani ya Bodi anawaomba wapige simu namba 0738441972 na 
 kwa masuala ya usajili wa Kitaaluma tupigie simu  namba 0738441971  kuanzia saa mbili kamili asubuhi mpaka saa kumi kamili jioni siku za kazi.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad