HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 24, 2019

PSPTB yaandaa mafunzo kwa Wataalamu wa Ununuzi na ugavi kutoka Taasisi za Serikali na binafsi

Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imeaanda mafunzo ya Siku mbili kwa  wataalamu wa ununuzi na ugavi kutoka taasisi za serikali na binafsi kuhusu upendeleo wa makundi maalumu kwenye sheria ya ununuzi wa umma.

Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Paul Bilabaye amesema serikali imeweka kifungu maalumu kinachozitaka taasisi nunuzi kutengeneza asilimia 30 ya ya bajeti zao za manunuzi kwenda kwa wanawake, Vijana,wazee na watu wenye ulemavu.

Bilabaye amesema, sheria hiyo inalenga kuwaandaa vijana ambao hawana ajira, wajiweke kwenye Makundi maalumu ili kujipatia kazi za ununuzi kutoka kwenye taasisi za umma.

Mafunzo hayo yamewakutanisha wataalamu wa ununuzi na ugavi kutoka taasisi za serikali na binafsi, Wajumbe wa bodi za zabuni na taasisi za umma zilizotajwa na sheria (Special Group Supporting Entity) ili kuzijengea uwezo wanamna bora ya kuyaandaa makundi maalumu ili yaweze kushiriki kwenye zabuni.
 Mwezeshaji wa mafunzo kutoka Mamlaka ya Rufaa ya Zabuni za Umma ( PPAA), Hamis Tika  akitoa mafunzo kwa wataalamu wa ununuzi na ugavi kutoka Taasisi za serikali na binafsi waliofika kwenye mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) yanayofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. 
 Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Paul Bilabaye(kushoto) akitolea ufafanuzi baadhi ya hoja zilizoibuliwa na mafunzo kwa wataalamu wa ununuzi na ugavi kutoka Taasisi za serikali na binafsi waliofika kwenye mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa PSPTB. Kulia ni Afisa Mwandamiza Masoko na mahusiano kwa Umma wa PSPTB, Shamim Mdee.
 Baadhi ya washiriki wakichangia mada kwenye mafunzo kwa wataalamu wa ununuzi na ugavi kutoka taasisi za serikali na binafsi waliofika kwenye mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB).

 Wataalamu wa ununuzi na ugavi kutoka Taasisi za serikali na binafsi, Wajumbe wa bodi za zabuni na taasisi za umma wakifuatilia mada kwenye mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB).
Wataalamu wa ununuzi na ugavi kutoka Taasisi za serikali na binafsi, Wajumbe wa bodi za zabuni na taasisi za umma wakiwa kwenye picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad