HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 6, 2019

NEC YATANGAZA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA SINGIDA MASHARIKI KUFANYIKA 31 JULAI, 2019

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetoa ratiba ya Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Singida Mashariki baada ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai kuitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge katika Jimbo la Singida Mashariki katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Mahakama ya Rufaa) Semistocles Kaijage alisema kuwa alitoa ratiba ya Uchaguzi huu Mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki kutokana na barua ya Spika wa Bunge inayoeleza kuwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Mheshimiwa Tundu Antipas Lissu kapoteza sifa ya kuwa Mbunge kutokana na kushindwa kuwasilisha kwa Spika tamko la mali na madeni na kushindwa kuhudhuria mikutano saba (7) mfululizo ya Bunge bila ruhusa ya Spika.

Mwenyekiti wa Tume, Kaijage, alizingati  matakwa ya kifungu cha 37 (1) (b) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343, kutoa taarifa kwa Umma kuhusu uwepo wa Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Singida Mashariki.

Jaji Kaijage kwa kuzingatia Katiba ya nchi na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi alifafanua ratiba ya Uchaguzi Mdogo huu kwa kueleza kuwa, Fomu za Uteuzi wa Wagombea zitatolewa kati ya  tarehe  13 hadi 18 Julai mwaka huu, Uteuzi wa Wagombea utafanyika tarehe  18, Julai mwaka huu na Kampeni za Uchaguzi zitafanyika kuanzia tarehe 19 hadi tarehe 30 Julai 2019 na Siku ya Uchaguzi itakuwa ni tarehe 31  Julai, 2019.

Aidha, Mwenyekiti, Jaji Kaijage alivikumbusha Vyama vya Siasa na wadau wote wa Uchaguzi kuzingatia Sheria, Kanuni, Maadili ya Uchaguzi, Taratibu, Miongozo na Maelekezo yanayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa kipindi chote cha Uchaguzi huu mdogo. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad