HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 29 July 2019

Naibu Waziri Shonza apongeza uongozi wa Kanisa la Baptist

Naibu Waziri Mhe.Juliana Shonza (kushoto) akimkabidhi zawadi ya mchezaji bora mchezaji kutoka Timu ya Yanga Mrisho Ngassa (kulia) mara baada kumalizika kwa mechi ya Tamasha la Michezo lililoandaliwa na Kanisa la Baptism la mkoa huo nakufanyika leo katika uwanja wa Jamhuri. 
Naibu Waziri Mhe.Juliana Shonza akimkabidhi kocha wa timu ya Mawenzi Market (ambaye jina lake halikufamika) zawadi ya mchezaji bora wa timu hiyo kwa niaba ya mchezaji huyo mara baada ya kumalizika kwa mechi yao iliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro,katikaTamasha la Michezo lililokuwa limendaliwa na kanisa la Baptist la Mkoani huo.
Naibu Waziri Mhe.Juliana Shonza (kushoto) akiteta jambo na Mchungaji Jerry Watt wa Kanisa la Baptist la Mkoani Morogoro aliyeandaa Tamasha la Michezo wakati wa mechi kati ya Timu ya Yanga na Timu ya Mawenzi Market ya Mkoani hapo walipokuwa wakicheza leo katika Uwanja wa Jamhuri.
Mchungaji wa Kanisa la Baptist la Mkoani Jerry Watt akihubiri neno la mungu katika Tamasha la Michezo lililofanyika leo katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro,Tamasha hilo liliandaliwa na kanisa hilo na lilikuwa na mechi kati ya timu ya Yanga na timu ya Mawenzi Market ya mkoa huo.
Naibu Waziri Mhe.Juliana Shonza akitizama kombe la ushindi kabla ya kulikabidhi kwa timu ya Yanga baada ya kuibuka washindi katika Tamasha la Michezo lililoandaliwa na kanisa la Baptist Michezo la Mkoa wa Morogoro na kufanyika leo katika Uwanja wa Jamhuri.
Kwaya ya Kanisa la Baptist kutoka Marekani ikiimba wimbo wakumsifu mungu katika Tamasha la Michezo lililoandaliwa na Kanisa hilo leo katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad