HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 2, 2019

MKUTANO WA 23 WA TAASISI ZA MAWASILIANO AFRIKA MASHARIKI (EACO) WAANZA JIJINI MWANZA

MKUTANO wa 23 wa Taasisi zinazosimamia Mawasiliano kwa Nchi za Afrika Mashariki, (EACO) umeanza leo Julai 1, 2019 jijini Mwanza.

Sambamba na mkutamno huo pia wajumbe watashiriki Mkutano Mkuu wa 26 wa EACO ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kuiweka Afrika Mashariki katika eneo la Uchumi wa Kidijitali".Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi, Atashasta Nditiye, ndiye aliyefungua mkutano huo utakaodumu hadi Julai 5, wenyeji ni Tanzania, pamoja na mataifa mengine ya WAC, ambayomni Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (wapili kushoto), akiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasilkiano Tanzania (TCRA), Mhandisi James M. Kilaba (watatu kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya  (TCRA), Dkt. Jones Killimbe (wanne kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa EACO  Dtk. Ally Yahya Simba(wakwanza kulia) na  Mwakilishi wa Katibu Mkuu Mawasiliano Bw.Mulembwa  Munaku. (wakzwanza kushoto),  baada ya kufungua mkutano wa 23 wa Taasisi zinazosimamia Mawasiliano Afrika Mashariki (EACO),  utakaofuatiwa na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 26 wa EACO jijini Mwanza Julai 1, 2019
Muwakilishi wa Umoja wa Shirika la Posta Duniani (upu), Kusini mwa Afrika na Asia, Bi. Gladys Mutyavaviri ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa upu, akizungumza kwenye mkutano huo wakati wa ufunguzi.
 Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James M. Kilaba, akizungumza na waandishi wa habari kufafanua baadhi ya mambo kuhusu mkutano huo.
 Wajumbe kutoka Burundi, wakisikilzia hotuba ya Mhe. Naibu Waziri.
 Wajumbe kutoka Kenya, wakisikilzia hotuba ya Mhe. Naibu Waziri.
 Wajumbe kutoka Rwanda, wakisikilzia hotuba ya Mhe. Naibu Waziri.
 Wajumbe wenyeji Tanzania, wakimsikiliza Mhe. Naibu Waziri Mhandisi Nditiye wakati akifungua mkutano huo.
Wajumbe kutoka Uganda, wakisikilzia hotuba ya Mhe. Naibu Waziri.
Mhe. Naibu Waziri Mhandisi Nditiye na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka mataifa wanachama wa EACO.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad