HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 23, 2019

MKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI MKOANI PWANI AMEZITAKA HALMASHAURI KUFUATA UTARATIBU WA MANUNUZI NA FEDHA

 NA MWAMVUA MWINYI, KIBITI
MKAGUZI wa hesabu za serikali mkoani Pwani, Hamis Juma amewataka wakuu wa idara ,maofisa ununuzi na wakuu wa vitengo ikiwemo cha fedha ,kuhakikisha wanafuata utaratibu wa manunuzi,fedha na sheria zilizowekwa ili kuondokana na kutofungwa kwa baadhi ya hoja na hati chafu.

Aidha amewataka ,kila mmoja asimame katika nafasi yake kusoma sheria zinazomuongoza katika idara yake.

Akizungumza katika baraza maalum la madiwani,huko Kibiti lililohusu kujadili taarifa za mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Juma alieleza halmashauri ya Kibiti ni moja ya halmashauri tisa mkoani hapo ambazo zilikuwa na hoja za miaka ya nyuma na hoja za mwaka husika 2017/2018.
 Alisema, halmashauri nyingi zimekuwa na hoja zisizofungwa kutokana na kutofuata taratibu na ukaguzi waliouweka.

Juma alifafanua kwamba, pia kutokuwa na ushirikiano baina ya halmashauri, watendaji na madiwani inasababisha utekelezaji wa kufunga hoja kukwama.

"Kumekuwepo na changamoto ya kiutendaji katika raslimali watu na fedha na kusimamia miradi ya maendeleo":Hivyo basi wakurugenzi na watendaji katika halmashauri zote tisa simamieni ili sheria,kanuni na taratibu zifuatwe kwa lengo la kusaidia mkaguzi akipita kusiwepo na dosari"alifafanua Juma.
Nae katibu tawala wa mkoa wa Pwani, Theresia Mmbando alisema ,watendaji wafuatilie na wawe wasimamizi na wazingatie sheria,kanuni na taratibu kwani ni suala la msingi katika utendaji kazi wao.

Alisema katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo fedha zinazokuwa hazijatumika wahakikishe wanatumia kwa mwaka husika na kwa makusudi yaliyolengwa.

Awali mkurugenzi wa halmashauri ya Kibiti ,Alvera Ndabagoye alisema kuwa wataendelea kufanya kazi kulingana na sheria,kanuni pamoja na kusimamia fedha za maendeleo zitumike kwa maslahi ya jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad