HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 30 July 2019

KAMPENI YA NSSF NA MARAFIKI YAVUNA WANACHAMA WAPYA

Meneja Kiongozi Mahusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Lulu Mengele akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wa kampuni ya KK Security wakati wa zoezi la kuwasajili. 
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeendelea kuandikisha wanachama wapya kutoka kwenye sekta binafsi na sekta isiyokuwa rasmi kupitia kampeni ya NSSF na Marafiki iliyoanzishwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kupitia kampeni hiyo NSSF imeweza kuandikisha wanachama wapya 472 kutoka katika kampuni ya KK Security. Kampuni ya ulinzi ya KK security ilishukuru NSSF kwa kuwapatia elimu ya hifadhi ya jamii kupitia kampeni ya NSSF na Marafiki iliyofanikisha kusajili wafanyakazi 472 na NSSF.

Kampeni ya NSSF na Marafiki itazunguka Tanzania nzima kwa lengo la kuandikisha wanachama wapya kutoka katika sekta binafsi na sekta isiyokuwa rasmi na kuhakikisha waajiri wanawasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati.

Kufuatia mabadiliko ya sheria ya hifadhi ya Jamii ya mwaka 2018 NSSF inatoa huduma ya Hifadhi ya Jamii kwa Sekta binafsi na Sekta Isiyokuwa Rasmi. Hivyo, Kampeni hii itasaidia kuongeza wanachama kutoka katika sekta hizo.
Meneja Kiongozi wa Uendeshaji wa NSSF, Cosmas Sasi (kulia) akimuelekeza jinsi ya kujaza fomu mfanyakazi wa Kampuni ya ulinzi ya KK Security wakati wa zoezi la kuandikisha wanachama wapya 472 wa kampuni ya KK Security jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa NSSF mkoa wa Kinondoni Hiza Kiluwasha wakati akijaza taarifa za mwanachama mpya wa NSSF katika mifumo ya kielektroniki ya Shirika.
Meneja Kiongozi wa Uendeshaji wa NSSF, Cosmas Sasi (kulia) akifuatilia maelekezo anayopewa mwanachama mpya wa NSSF ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya ulinzi ya KK Security wakati wa zoezi la kuandikisha wanachama wapya kampuni ya KK Security jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad