HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 17, 2019

KANYASU AWASHAURI WAKULIMA WA PAMBA WASIUZE PAMBA KWA WALANGUZI

Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewashauri  Wakulima wa zao la pamba wawe wavumilivu badala ya kuuza pamba hiyo kwa walanguzi kwa bei ya chini  huku Serikali ikiendelea kuwatafutia soko zuri.

Amesema Serikali ilishaahidi kuwa kama pamba hiyo haitanunuliwa  kwa bei elekezi ya kilo moja kwa shilingi 800 hadi mwezi Agosti mwaka huu basi Serikali itainunua pamba hiyo ili kuwafidia wakulima hao.

Hatua  hiyo inakuja kufuatia Wafanyabiashara wengi  kushindwa kununua kwa bei hiyo  kutokana bei ya soko la pamba duniani kuporoka.

Akizungumza kwenye mkutano uliofanyika katika eneo la Kasamwa mkoani Geita, Mhe.Kanyasu amesema   wafanyabiashara wameshindwa  kukopa pesa benki kwa ajili ya kuinunua pamba hiyo kutokana na kukosekana kwa soko la kuiuza.

Mhe.Kanyasu amesema kufuatia hali hiyo baadhi ya wakulima wamekuwa wakiiuza pamba hiyo kwa shilingi 500 kwa kilo moja kwa walanguzi hali inayowadidimiza kiuchumi.

Ametaja mikakati ambayo tayari Serikali imeshaichukua ikiwemo kuzungumza na Serikali ya Vietnam ambao tayari wameonesha nia ya kununua pamba hiyo kwa Wakulima.

Aidha, Mhe Kanyasu amewaeleza Wakulima hao kuwa Waziri wa Kilimo anatambua tatizo hilo na ameahidi kutembelea mkoa huo kwa ajili ya kuzungumza na Wakulima hao.

Naye Juma Kaludushi ambaye ni mkulima wa zao pamba amesema wakulima walio wengi akiwemo na yeye wamekuwa wakiuza pamba hiyo kwa walanguzi kwa bei ya chini kwa hofu kuwa pamba hiyo itaharibika mikononi mwao.

"Pamba ipo majumbani mwetu muda unakwenda bora tuuze tu kwa Walanguzi ili isiharibike kuliko tukapata hasara kabisa" Amesema Mkulima huyo.


Kwa upande wake, Ester Nalamo, ambaye ni Mkulima wa pamba amesema  amelazimika kuuza pamba  kwa bei ya chini ili aweze kuwalipia ada watoto wake kwa vile yeye hana chanzo kingine cha mapato zaidi ya kuuza pamba.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Geita mjini Mhe.Constantine Kanyasu akiwa na Diwani wa viti maalum, Jesca Kalalio wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Kasamwa mkoani Geita ambapo pamoja na mambo mengine Mhe, Kanyasu aliwaeleza wananchi hao kuhusiana na  jitihada mbalimbali  zinazofanywa na Serikali za kutafuta soko zuri kwa ajili ya zao la pamba.
 Baadhi ya wananchi wa Kata ya Kasamwa waliokusanyika katika eneo la mkutano kwa ajili ya kumpokea Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Geita mjini Mhe.Constantine Kanyasu mara baada ya kuwasili katika eneo la mkutano.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Geita mjini Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza nan wananchi kwenye mkutano wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Kasamwa mkoani Geita ambapo amewashauri wakulima wasiuze pamba yao kwa walanguzi ambao wamekuwa wakinunua kwa bei ndogo.
 Wananchi wa Kata ya Kasamwa wakimsiliza Mbunge wao, Mhe. Constantine Kanyasu wakati wa mkutano uliofanyika mkoani Geita ambapo amewataka kuwa wavumilivu huku Serikali ikiendelea kuwatafutia soko la zao la pamba.
 Mwenyekiti wa  CCM wa wilaya ya Geita, Bw. Barnabas Mapande akizungumza na wananchi wa Kata ya Kasamwa kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Geita mjini Mhe.Constantine Kanyasu kwa ajili ya kuzungumza nao.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Geita mjini Mhe.Constantine Kanyasu (katikati) akiwa na baadhi ya viongozi wa CCM pamoja na watumishi wa Umma mara baada ya mkutano wa hadhara kufunguliwa katia kata ya Kaswama mkoani Geita.
 Diwani wa Kata ya  Kanyala, Mhe. Logaloga akizungumza na wananchi kwa jinsi anavyoshirikiana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Geita mjini Mhe.Constantine Kanyasu katika kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo la Geita mjini.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Geita mjini Mhe.Constantine Kanyasu akiwatambulisha Makatibu wake kwa wananchi wa Kata ya Kasamwa mara baada ya kuzungumza na wananchi hao mamabp mbalimbali ikiwemo bei ya pamba, ufumbuzi wa suala  la maji na nishati ya umeme

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad