HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 13, 2019

KAMATI YA UONGOZI YA JUMUIYA YA MADOLA KANDA YA AFRIKA YAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM

 Spika wa Bunge la Kenya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Mhe. Justin Muturi akiongoza kikao cha Kamati hiyo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam mapema leo. Wa kwanza Kulia ni Katibu wa CPA-Kanda ya Afrika na ambaye pia ni Katibu wa Bunge la Tanzania Ndg. Stephen Kagaigai na  wanaofuatia upande huo ni Wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati hiyo  . Upande wa kushoto ni Wajumbe wa Kamati hiyo na ambao pia ni Wabunge kutoka Zambia, Uganda,Namibia, Ghana na Kenya.
 Spika wa Bunge la Kenya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Mhe. Justin Muturi akiongoza kikao cha Kamati hiyo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam mapema leo.  Wakwanza kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Cameroon Mhe. Emilia Lifaka.  Pia, wanaofutia upande huo ni Wajumbe wa Kamati hiyo kutoka Bunge la Zambia, Uganda na Namibia.
  Katibu wa CPA-Kanda ya Afrika na ambaye pia ni Katibu wa Bunge la Tanzania Ndg. Stephen Kagaigai (wa kwanza kulia) akizungumza wakati wa kikao hicho.
 Spika wa Bunge la Kenya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Mhe. Justin Muturi akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Cameroon Mhe. Emilia Lifaka alipowasili kwa ajili ya kikao hicho. PICHA NA BUNGE

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad