
Wajasiriamali Wamachinga sasa kuanza
kunufaika na mikopo ya kidijitali kutoka Benki ya CRDB kufuatia urasimishwaji
wa kundi hilo uliofanywa na Serikali nchi nzima kupitia vitambulisho vya
ujasirimali.
Akizungumza kuhusiana na fursa hiyo wakati wa Semina ya Wajasiriamali
kwa Mkoa wa Morogoro iliyofunguliwa na Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Kebwe
Steven, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela
amesema huduma hiyo ya mikopo ambayo itapatikana kupitia mfumo wa
SimAccount inalenga katika kuwajengea uwezo wajasiriamali wadogo nchini
kukuza biashara zao.
“Mikopo hii itakuwa ikipatikana kwa mfumo wa kidijitali kupitia huduma yetu ya
SimAccount, hii itawezesha wateja kupata mikopo kwa haraka zaidi kupitia
simu zao za mkononi bila kutembelea tawini. Tunafanya hivi tukijua uhitaji wa
mikopo kwa kundi hili la wateja ni mkubwa na mara nyingi wamekuwa na
uhitaji wa haraka,” alisema Ndugu Nsekela.
Ndugu Nsekela alisema Benki ya CRDB imekuwa ikitoa kipaumbele kwa
kundi la wajasiriamali katika mpango mkakati wake wa biashara ambapo
benki imekuwa ikibuni huduma na bidhaa maalum kwa ajili ya kundi hilo
ikiwemo mikopo. “Kwa mwaka jana pekee tumefanikiwa kutoa mikopo ya
jumla ya shilingi bilioni 421.58 kwa wateja wetu wajasiriamali”, aliongezea
Ndugu Nsekela.
Dkt. Kebwe ameipongeza Benki ya CRDB kwa hatua hiyo akisema hatua hiyo
itasaidia kutimiza juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais
Dkt. John Pombe Magufuli katika kuwawezesha wajasiriamali wamachinga
nchini kupiga hatua katika biashara zao ikiwa ni mkakati wa kuwainua
kiuchumi kufikia Tanzania yenye uchumi wa kati.
Dkt. Kebwe alitumia fursa hiyo pia kuipongeza Benki ya CRDB kwa kuwa
mstari wa mbele katika kukuza sekta ya kilimo nchini kupitia bidhaa yake ya
FahariKilimo.
Dkt. Kebwe aliwataka wajasiriamali na wafanyabiashara
waliohudhuria katika semina hiyo kuchangamkia fursa ya mikopo ya kilimo
inayotolewa na Benki ya CRDB, huku akieleza kuwa mkoa wa Morogoro
unafursa kubwa ya kimaendeleo kupitia sekta ya kilimo hususani kilimo cha
miwa, mpunga, pamba, korosho na kahawa.
Mbali ya kupata mafunzo juu ya fursa mbalimbali za ukuzaji biashara kupitia
huduma na bidhaa mbalimbali za Benki ya CRDB, Wajasiriamali hao pia
walipata fursa ya kutoa maoni juu ya uboreshwaji wa huduma.
Hivi karibuni Benki ya CRDB imetoa kiasi cha dola za kimarekani 60,000
kudhamini tafiti ya kampuni bora 100 ikijikita katika kipengele cha wajasirimali
ambacho ni muhimu katika maendeleo ya kiuchumi na kuchochea makampuni
hayo kufanya vizuri zaidi.
Mkuuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven akisaliamiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati alipowasili katika Semina ya Wajasiriamali iliyoandaliwa na Benki ya CRDB, katika hoteli ya Nasheera, Mkoani Morogoro, Julai 13, 2019. Katikati ni Meya wa Manispaa ya Morogoro Pascal Kihanga.
Mkuuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven akiwa ameongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati alipoingia katika ukumbi tayari kwa Semina ya Wajasiriamali iliyoandaliwa na Benki ya CRDB, katika hoteli ya Nasheera, Mkoani Morogoro, Julai 13, 2019.
Mkuuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven akitoa hotuba yake wakati akifungua Semina maalum kwa Wajasiriamali iliyoandaliwa na Benki ya CRDB, , katika ukumbi wa hoteli ya Nasheera, Mkoani Morogoro, Julai 13, 2019.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza na wafanyabiashara wa mkoa wa Morogoro juu ya fursa mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo kwa wafanyabiashara katika Semina maalum kwa wajasiriamali iliyoandaliwa na benki hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Nashera mkoani Morogoro, Julai 13, 2019.
Meya wa Manispaa ya Morogoro Mh. Pascal Kianga akizungumza na wafanyabiashara wa mkoa wa Morogoro juu ya furs mbalimbali zinazotolewa na bench hiyo kwa wafanyabiashara katika Semina maalum kwa wajasiriamali iliyoandaliwa na benki hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Nashera,
No comments:
Post a Comment