Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwakaribisha Zanzibar Madaktari Mabingwa Wapya na kuwaaga wale waliomaliza Muda wao Mwaka Mmoja wa kutoa huduma za Afya wanaotoka Nchini Jamuhuri ya Watu wa China.
Naibu Katibu Mkuu Wizara wa Afya Zanzibar Bibi Halima Salum Maulid akifafanua mafanikio ya huduma za Afya kutokana na uwepo wa Madaktari mabingwa kutoka China.
Balozi Seif akipokea zawadi kutoka kwa Kiongozi wa Madaktari Mabingwa kutoka Jauhuri ya Watu wa China waliomaliza Muda wao hapa Zanzibar Dr. Zhang Zhen
Balozi Seif kati kati waliokaa vitini katika katika picha ya pamoja na Madaktari Mabingwa Wapya na kuwaaga wale waliomaliza Muda wao Mwaka Mmoja wa kutoa huduma za Afya wanaotoka Nchini Jamuhuri ya Watu wa China.
Timu ya Madaktari Mabingwa Wapya na kuwaaga wale
waliomaliza Muda wao wa China wakiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatafakari kuangalia uwezekano wa
kuiomba Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kuwaongezea muda wa
kutoa huduma za Afya Madaktari wa Nchi hiyo wanaopangiwa kufanyakazi
katika Hospitali za Rufaa hapa Zanzibar.
Alisema kutokana na ukarimu na huduma bora za Madaktari hao
wanazozitoa kwa Wananchi upo umuhimu wa kuombewa muda wa Miaka Miwili
badala ya ule Mmoja uliozoeleka katika Mkataba uliosainiwa kati ya
Serikali hizo mbili mnamo Mwaka 1965.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar
wakati akiwakaribisha Zanzibar Madaktari Mabingwa Wapya na kuwaaga
wale waliomaliza Muda wao Mwaka Mmoja wa kutoa huduma za Afya kutoka
Nchini Jamuhuri ya Watu wa China.
Alisema Jamii ya Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla tayari
wanazikubali huduma zinazotolewa na Madaktari Bingwa kutoka Nchini
China kiasi kwamba uwepo wao katika kipindn cha Mwaka Mmoja
kinaonyesha kutokidhi kiu na mahitaji halisi ya Wananchi hao katika
kupata huduma hiyo.
Alisema licha ya mazingira ya kupendeza kuona Madaktari wakongwe
wanaondoka na wapya wanaingia kwa wakati katika kutoa matibabu ya
Maradhi mbali mbali lakini bado muda wa ziada kwa mabingwa hao
unahitajikja kwa vile tayari wameshakuwa kama Wana Jamii.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliishukuru na kuipongeza Serikali
ya Jamuhuri ya Watu wa China kwa moyo wake wa kuendelea kuiunga mkono
Zanzibar katika Sekta ya Afya.
Mapema Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Hamad Rashid Mohamed alisema
iliyoingia Nchini hivi sasa ni Timu ya 29 ya Madaktari Mabingwa wa
China ikiwa ni mfumo maalum ulioasisiwa tokea Mwaka 1965 wa kuwapokea
Wataalamu hao kwa lengo la kutoa huduma za Afya Zanzibar.
Mh. Hamad alisema Timu ya Madaktari ya Awamu ya 28 ilifanya kazi kubwa
kama zilivyofanywa zile zilizotanguliwa kazi ambayo inastahiki
kuendelezwa na Timu Mpya iliyoingia Nchini kushika dhamana hiyo.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Madaktari Mabingwa wa China waliomaliza
Muda wao Kiongozi wa Madaktari hao Dr. Zhang Zhen alisema Timu hiyo
imefanya kazi kubwa iliyoelata mafanikio makubwa kutokana na
ushirikiano walioupata kutoka kwa Madaktari Wazawa.
Dr. Zhang alisema katika utumishi wao wa Mwaka Mmoja waliokuwepo
Zanzibar Mabingwa hao wameweza kukabiliana na kesi 100 zilizokuwa
zikiwasumbua Wananchi na kuzipatia ufumbuzi wa Kitaaluma.
Alisema Mabingwa hao waliomaliza muda wao walikuwa na mpango Maalum
uliowawezesha kutoa huduma za Afya katika Hospitali mbali mbali za
Mikoa, Wilaya hadi Vijijini.
Alifahamisha kwamba huduma hizo zilikwenda sambamba na utolewaji wa
mafunzo kwa Madaktari Wazalendo pamoja na Semina zilizoshirikisha
Watendaji wa Afya pamoja na wale wanaohusika na utoaji wa huduma ya
kwanza.
No comments:
Post a Comment