'WE FARM' WAJA NA HUDUMA ZA KIDIGITALI KUWASAIDIA WAKULIMA TANZANIA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 27 June 2019

'WE FARM' WAJA NA HUDUMA ZA KIDIGITALI KUWASAIDIA WAKULIMA TANZANIA

Katika kuhakikisha wakuliwa mbalimbali nchini wanapata taarifa za kilimo na kukifanya kiwe na tija, taasisi isiyo ya kiserikali iitwayo ‘We Farm’ imenzisha mradi unaowaunganisha wakulima kuwasiliana moja kwa moja na kupeana taarifa zitakazowawezesha kutimiza mahitaji yao ya kilimo.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam Meneja Mkuu wa taasisi hiyo Nicholus John amesema ujio wa ‘We Farm’ zaidi umelenga kutatua changamoto zinazowakabili wakulima ikiwemo kukosa taarifa sahihi zinazohusiana na masuala ya kilimo hicho na kuwafanya wapate hasara kwa kukosa au mazao wanayoyalima kutokidhi makusudio yao.

Amesema mradi huo uliolenga kuwafikia wakuliza 400,000 ifikapo mwisho wa mwaka huu, zaidi utawaunganisha wakulima hao lupitia simu zao za mikononi huku ukitumia mwanya huo pia kupata majibu ya maswali mbalimbali yanayohusiana na kilimo wanachokifanya.

Nicholus amesema katika utekelezaji wa majukumu yake, ‘We Farm’ pia itafanya kazi kwa karibu na maafisa wa ugani waliopo katika halmashauri zote nchini ili kuleta tija zaidi katika kilimo hicho na hivyo kukuza uchumi wao pamoja na wa taifa kwa ujumla.

“Huduma hii inawawezesha wakulima kuwasiliana wao kwa wao na kuelezana changamoto zilizopo katika kilimo na kupaena majibu juu ya maswali mbalimbali yanayojitokeza, kikubwa ‘we farm’ ni ukumbi wa majadiliano kwa wakulima” aliongeza Nicholus.

Aidha amesema utafiti walioufanya hivi karibuni walibaini uwepo wa changamoto ya ukosefu wa taarifa kwa wakulima hao na hivyo kuwafanya washindwe kupata majibu katika masuala mbalimbali yanayohusiana na kilimo hicho.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya ufuatiliaji wa taasisi hiyo Cyrila Anton amesema kupitia huduma hiyo, wakulima wataweza kupiga hatua katika kilimo wanachokifanya na hivyo kuwawezesha kupata mafanikio yanayotokana kilimo wanachokifanya.
Meneja Mkuu wa taasisi ya 'We Farm' Bw. Nicholus John akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam waliofika katika mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya kuijua taasisi hiyo na malengo yake katika kutoka huduma kwa wakulima nchini Tanzania. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakisikiliza mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo.
Mkuu wa Idara ya ufuatiliaji wa taasisi ya We Farm Bi. Cyrila Anton akitoa ufafanuzi zaidi masuala mbalimbali ya wakulima.
Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakisikiliza mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo.
Mmoja ya viongozi akiuliza maswali.
Viongozi wa taasisi ya We Farm wakiwa katika picha ya pamoja na wahariri wa vyombo vya habari mara baada ya kumaliza mafunzo ya kuwajenga uwezo. Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad