HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 27, 2019

WAZIRI MHAGAMA APOKEA MSAADA WA VIFAA SAIDIZI NA CHEREHANI KUTOKA UBALOZI WA CHINA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amepokea cherehani na vifaa siadizi kwa ajili ya Watu wenye Ulemavu vilivyotolewa na Ubalozi wa China nchini.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi ndogo za ubalozi huo zilizopo Jijini Dodoma, Waziri Mhagama alieleza kuwa Serikali inatambua haki za Watu wenye Ulemavu nchini hivyo imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata haki zao stahiki ikiwemo kuwapatia vifaa saidizi.

“Vifaa saidizi ni muhimu kwa kundi hilo maalumu kwa kuwa vinawawezesha kumudu mazingira yanayowazunguka na kuwasaidia kufanya shughuli zao za kila siku bila kukabiliana na changamoto,” alisema Mhe. Mhagama

Alieleza kuwa kutokana na vifaa hivyo kuwa ni ghali na upatikanaji wake umekuwa mgumu na kupelekea watu wenye ulemavu kushindwa kuvinunua, Serikali imeendelea kutenga bajeti kwa ajili ya kununua vifaa hivyo.

Aliongeza kuwa, katika ujenzi wa uchumi wa viwanda Serikali kupitia Shirika la kuhudumia viwanda Vidogovidogo (SIDO) kushirikiana na wadau imejipanga kuimarisha utengeneza wa baadhi ya vifaa hivyo, vitakavyokuwa vinapatikana hapa nchini.

Aidha alitoa wito kwa jamii kubadili mtazamo na fikra potofu juu ya watu wenye ulemavu, bali watambue kundi hilo linaweza na linamchango mkubwa katika jamii na nchi kwa ujumla.

Kwa upande wake, Balozi wa China nchini Tanzania, Bi. Wang Ke alisema kuwa Serikali ya China itaendelea kuimarisha ushirikiano wake na Serikali ya Tanzania katika nyanja mbalimbali pamoja na kuendelea kutoa misaada kwa ajili ya wenye uhitaji.

Naye Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa aliwataka wadau ndani na nje ya nchi kuendelea kujitokeza na kusaidia makundi yenye uhitaji maalumu, kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kusaidia masuala ya Watu wenye Ulemavu.

Katika hafla hiyo pia aliudhuria Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mhe. Fatma Toufiq na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza Mhe. Kemilembe Lwota.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Vifaa saidizi kwa ajili ya Watu wenye Ulemavu na Cherehani kwa ajili ya wakina Mama zilizotolewa na Balozi wa China Nchini Bi. Wang Ke wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo tarehe 26 Juni, 2019 katika Ofisi ndogo za Ubalozi huo zilizopo Jijini Dodoma.
 Balozi wa China Nchini Tanzania Bi. Wang Ke akielezea namna Serikali ya China imekuwa ikisaidia masuala mbalimbali nchini wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Vifaa saidizi kwa ajili ya Watu wenye Ulemavu na Cherehani kwa ajili ya wakina Mama iliyofanyika Jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiteta jambo na Balozi wa China Nchini Tanzania Bi. Wang Ke wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Vifaa saidizi kwa ajili ya Watu wenye Ulemavu na Cherehani kwa ajili ya wakina Mama iliyofanyika Jijini Dodoma katika Ofisi ndogo za Ubalozi huo Juni 26, 2019.
 Baadhi ya Viongozi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama. Kushoto ni Balozi wa China Nchini Tanzania Bi. Wang Ke, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mhe. Fatma Toufiq(kulia).
 Baadhi ya Wadau walioshiriki kwenye hafla hiyo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani).
 Sehemu ya washiriki katika hafla hiyo iliyofanyika katika Ofisi ndogo za Ubalozi wa China zilizopo Jijini Dodoma. 
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) pamoja na Balozi wa China Nchini Tanzania Bi. Wang Ke (katikati) wakimkabidhi Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa (kulia) Kiti Mwendo “Wheelchair” ikiwa ni sehemu ya maabidhiano wakati wa hafla hiyo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (wa pili kutoka kulia) akimkabidhi Fimbo Nyeupe “White Cane” mmoja wa wanafunzi wasioona kutoka Shule ya Msingi ya Buigiri. Wa tano kutoka kulia ni Balozi wa China Nchini Tanzania Bi. Wang Ke. Kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa.
 Balozi wa China Nchini Tanzania Bi. Wang Ke akimkabidhi cherehani kwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mhe. Fatma Toufiq wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki (wa tatu kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa China Nchini Tanzania Bi. Wang Ke (katikati). Wa tatu kutoka kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza Mhe. Kemilembe Lwota na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mhe. Fatma Toufiq.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad