HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 12, 2019

NDITIYE: WMO INAMCHANGO MKUBWA KATIKA HUDUMA ZA HALI YA HEWA TANZANIA.

Na Christopher Philemon, Monica Mutoni. Geneva
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawsailiano Mhandisi Atashasta Nditiye ameeleza namna ambavyo Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) linavyochangia katika uboreshaji wa huduma za hali ya hewa Tanzania.Amezungumza hayo wakati akihutubia mkutano wa 18 wa WMO, unaoendelea jijini Geneva, Uswisi.

‘WMO ina mchango mkubwa katika huduma za hali ya hewa nchini kama vile miongozo maalum iliyowekwa kwa ajili ya uandaaji na utoaji wa tahadhari za hali mbaya ya hewa kwa maeneo ya ziwa Viktoria ambapo TMA inatoa miongozo ya tahadhari kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, utekelezaji wa Mfumo wa Kidunia wa Huduma za Hali ya Hewa (Global Framework for Climate Services-GFCS) ambao ndani yake Tanzania kupitia TMA inanufaika masuala mbalimbali kama vile mafunzo ya muda mrefu na mfupi, upatikanaji wa baadhi ya vifaa vya hali ya hewa  alisema’ Alisema  Nditiye. 

Aidha, katika hotuba yake, naibu waziri  Nditiye aliwasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na kuelezea namna Serikali inavyoweka jitihada kubwa kuhakikisha huduma za hali ya hewa nchini zinakuwa za kisasa kwa kufanikisha ununuzi wa rada tatu za hali ya hewa pamoja na kuifanya TMA iweze kukidhi zaidi matakwa ya watumiaji kwa kuibadilisha TMA kutoka kuwa Wakala na kuwa Mamlaka kamili.

Wakati akimalizia hotuba yake, Naibu waziri  Nditiye alitumia nafasi hiyo kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kumnadi mgombea wa nafasi ya makamu wa tatu wa Rais wa WMO Dkt. Agnes Kijazi kutokana na uwezo na uzoefu alionao WMO akiwa mjumbe wa kamati kuu wa shirika hilo kwa miaka saba.   
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawsailiano Mhandisi Atashasta Nditiye akihutubia mkutano wa 18 wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) mbele ya wajumbe kutoka nchi mbalimbali waliodhuria mkutano huo unaofanyika kila baada ya miaka 4(Picha Christopher Philemon)

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawsailiano Mhandisi Atashasta Nditiye akiwa na kaimu Balozi  Bw. Robert Kahendaguza , mkurugenzi mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi na baadhi ya waumbe kutoka Tanzania kwenye mkutano wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) unaofanyika Geniva (Picha na Christopher Philemon)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad