HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 27 June 2019

Mwenyekiti mpya wa bodi ya Airtel Tanzania PLC na Afisa mkuu mpya wa Ufundi kutoa ushirikiano kwa Uongozi kampuni hiyo

 Mwenyekiti mpya wa bodi ya Airtel Tanzania PLC Dkt Omary Nundu akisalimiana na Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Tanzania alipotembelea Makuu ya ya Airtel Tanzania yaliyopo jijini Dar es salaam mtaa wa Morocco. Mwenyekiti huyo ameahidi kushirikiana na uongozi kuhakikisha kampuni hiyo inayomilikiwa na watanzania kwa asilimia 49% inaleta tija kwa watanzania.
 Afisa Mkuu wa Ufundi mpya wa Airtel Tanzania Dkt Prospa Mafole (kati) na Mwenyekiti mpya wa bodi ya Airtel Tanzania PLC Dkt Omary Nundu (kulia) wakisalimiana na mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Bw, Sunil Colaso walipotembelea yaliyopo jijini Dar es salaam mtaa wa Morocco hivi karibuni. Mkuu huyo wa ufundi anaendelea na kazi sasa baada ya kuteuliwa na serikali ili kujiunga na uongozi uliopo wa Airtel kuhakikisha kampuni hiyo inayomilikiwa na watanzania kwa asilimia 49% inatoa huduma bora zaidi na kuipa serikali mwekezaji faida .
 Mwenyekiti mpya wa bodi ya Airtel Tanzania PLC Dkt Omary Nundu (kulia) na Afisa mkuu mpya wa Ufundi Dkt Prospa Mafole wakisalimiana na Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Tanzania Sunili Colaso (kushoto) leo walipotembelea yaliyopo jijini Dar es Salaam mtaa wa Morocco. Mwenyekiti bodi na Afisa ufuni Mpya walioteuliwa na serikali kushika nyadhifa hizo wameahidi kushirikiana na uongozi kuhakikisha kampuni hiyo inayomilikiwa na watanzania kwa asilimia 49% inaleta tija kwa watanzania.
Wakwanza tokea kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Tanzania Sunil Colaso akifuatiwa na Mwenyekiti mpya wa bodi ya Airtel Tanzania PLC Dkt Omary Nundu na Afisa mkuu mpya wa Ufundi Dkt Prospa Mafole wakiwa kwenye kikao cha ukaribisho mara baada ya kutembelea Makuu ya Airtel Tanzania jijini Dar es Salaam mtaa wa Morocco leo na baadhi ya wakuu wavitengo mbalimbali wa Airtel Tanzania.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad