MBUNGE wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, James Ole Millya
amewashukuru wananchi wa Vijiji vya Sukuro na Kitiangare waliomaliza
mgogoro wao uliodumu zaidi ya miaka 20 wakigombea Kitongoji cha
Katikati.
Mgogoro huo ulishasababisha mtafaruku mkubwa baina ya aliyekuwa mkuu
wa mkoa huo Henry Shekifu na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo
Christopher Ole Sendeka mwaka 2010.
Ole Millya akizungumza na wananchi wa kijiji cha Sukuro na Kitiangare
aliwapongeza wananchi wa vijiji hivyo viwili kwa kuridhia kwa pamoja
na kuachana na malumbano na mgogoro usiokuwa na tija kwao.
Alisema katika mgogoro huo yeye binafsi alikaa pembeni bila kupendelea
kijiji chochote kwani vyote viwili ni vya kwake hivyo hakupaswa
kupendelea kimoja aliwaachia wataalamu wagawe vitongoji kama sheria
inavyoelekeza.
"Nawapongeza sana wananchi wa vijiji vya Kitiangare na Sukuro kwani
hali ya amani haikuwepo lakini sasa mmemaliza mgogoro wenu na kuridhia
kwa pamoja kuishi kama ndugu kwani mlikuwa kijiji kimoja kabla ya
kugawanywa," alisema Ole Millya.
Alisema hivi sasa hali ya amani na upendo imerejea baina ya vijiji
hivyo viwili kama awali na wananchi wanasalimiana kwa furaha,
wanaoleana na kunywa maji pamoja.
Alisema kupitia mfuko wa jimbo anatoa sh6 milioni kwa vikundi vya
wanawake wa vijiji vyote viwili na sh4 kwa mradi wa maji kijiji cha
Sukuro na darasa la shule ya kijiji cha Kitiangare.
Mkazi wa kijiji cha Sukuro, Lengai Ole Makoo alipongeza hatua ya
kumalizika kwa mgogoro huo usiokuwa na tija uliosababishwa na baadhi
ya wanasiasa wa wilaya hiyo.
Ole Makoo alisema kijiji cha Sukuro kimebakiwa na vitongoji vyake
vitano na kijiji cha Kitiangare kimebaki na vitongoji vyake viwili
kama ambavyo kanuni, taratibu na sheria zilivyofuatwa wakati kijiji
mama cha Sukuro kilipogawanywa.
"Kijiji cha Sukuro kimebaki na vitongoji vya Katikati, Lembutwa,
Lenjani, Mouwara na Lasepa na Kitiangare imebaki na vitongoji vya
Loongung na Kitiangare," alisema.
Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti alimpa onyo
Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Awadhi Omary na baadhi ya wanasiasa
juu ya kutumika kwa maslahi yao katika mgogoro huo.
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, James Ole Millya akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Sukuro alipotembelea eneo hilo.
Mbunge wa jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, James Ole Millya akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Kitiangare.
Mbunge wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, James Ole Millya
akizungumza juu ya upendo na kuondokana na makundi na ubaguzi ili
lengo la kuwa na Simanjiro moja yenye amani na kutobaguana itimie
No comments:
Post a Comment