HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 27, 2019

KAMISHNA MPYA TIRA DKT JUMA AKABIDHIWA OFISI RASMI LEO JIJINI DAR

Aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Dkt Baghayo Abdallah Saqware amekabidhi rasmi majukumu kwa Kamishna mpya Dkt Mussa Juma leo kwenye ofisi zao Jijini Dar es salaam.
Dkt Juma ameteuliwa mapema wiki hii na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ambapo uteuzi wake ulianza rasmi Juni 25, mwaka huu.
Kabla ya kuteuliwa kuchukua nafasi hiyo, Dkt Juma alikuwa Mkuu wa Idara ya Bima katika kitivo cha Bima na Hifadhi ya Jamii cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM). TIRA ni mamlaka ya inayosimamia  Bima zote nchini.
 Aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Dkt Baghayo Saqware(kulia) akikabidhi taarifa za ofisi kwa Kamishna mteule wa Mamlaka hiyo Dkt Mussa Juma kwenye ofisi zao leo Jijini Dar es Salaam. Dkt Juma ameteuliwa Juni 25 mwaka huu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
 Aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Dkt Baghayo Saqware(kushoto) akiweka saini kwenye nyaraka zenye taarifa za ofisi sambamba na Kamishna mteule wa Mamlaka hiyo Dkt Mussa Juma wakati wa makabidhiano ya majukumu kwenye ofisi zao leo Jijini Dar es Salaam. Dkt Juma ameteuliwa Juni 25 mwaka huu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Dkt Baghayo Saqware(kulia) wakikumbatiana na   Kamishna mteule wa Mamlaka hiyo Dkt Mussa Juma baada ya  makabidhiano ya majukumu kwenye ofisi zao leo Jijini Dar es Salaam. Dkt Juma ameteuliwa Juni 25 mwaka huu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad