HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 14, 2019

Copa America kuanza rasmi usiku wa kuamkia kesho


Michuano ya 46 ya Copa America inaanza rasmi usiku wa kuamkia kesho (Saa 9:00 Alfajiri) hadi Julai 7 ambapo mechi zitachezwa katika majiji matano nchini Brazil. Copa America itahusisha jumla ya timu kumi na mbili zikiwemo Japan na Qatar ambao wamealikwa kushiriki.

Brazil wameahi kuwa wenyeji wa michuano hiyo mara nne, na mar azote hizo wameweza kulibakisha kombe nyumbani. Usiku wa leo wanaanza kibarua cha kutunza rekodi hiyo watakapocheza mechi ya ufunguzi dhidi ya Bolivia saa 9:30 Alfajiri. Michuano hiyo itachezwa kwenye viwanja 6 katika majiji matano huku fainali ya Julai 7 ikipigwa katika dimba la Estadio de Maracana jijini Rio de Janeiro.

Timu 12 zinazoshiriki zimepangwa katika makundi matatu yenye timu nne kila moja, ambapo timu mbili za juu kwenye kila kundi zitaingia moja moja kwenye hatua ya mtoano huku timu mbili kwenye nafasi ya tatu lakini zina rekodi nzuri (best loser) zikiungana nazo kwenye hatua ya mtoano..

Brazil watamkosa mshambuliaji Neymar ambaye aliumia kifundo cha mguu kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Qatar. Hata hivyo bado wana kikosi kizuri chenye uwezo wa kulibakisha kwenye ardhi ya nyumbani. Lionel Messi ndiye atatupiwa macho na watu wengi, hii ikiwa ni nafasi yake ya dhahabu kushinda Kombe akiwa na timu ya taifa ya Argentina.

Japokuwa ameshinda kila taji akiwa na klabu ya Barcelona na mataji binafsi, Messi bado hajashinda kombe lolote akiwa na timu ya taifa (ya wakubwa) na muda ni kama unaelekea kumtupa mkono. Msimu huu Messi atakuwa na shauku ya kuongezea kwenye mataji 14 ambayo Argentina wamewahi kushinda.

Argentina wamepangwa katika kundi B pamoja na Colombia, Paraguay na mabingwa wa Bara Asia Qatar. Wataanza kampeni yao siku ya Jumapili saa 7:00 Usiku dhidi ya Colombia.
Chile wao wataanza michuano dhidi ya Japan siku ya Jumanne saa 8:00 Usiku.
Michuano hii inaonyeshwa na StarTimes pekee kupitia chaneli zao za michezo ambazo zipo katika mfumo wa HD, ST World Football HD, Sport Life HD, ST Sport Premium HD, Sports Arena HD na Sport Focus

Pia mechi zitapatikana LIVE kupitia application ya StarTimes ON kwa watumiaji wa simu janja. Kwa watumiaji wa dikoda za Antena Copa America itapatikana katika kifurushi cha MAMBO kwa Tsh 14,000 na wateja wa dikoda za dish kifurushi cha SMART kwa Tsh 21,000.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad